
“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Ukarimu
Jumatatu, Aprili 7, 2025.
Juma la 5 la Kwaresima
Dan 13:1-9,15-17,19-30,33-62;
Zab 23: 1-6;
Yn 8: 12-20.
KUTEMBEA NA MUNGU
Tunakaribia pasaka, kipindi cha ufufuko wa Bwana wetu. Maada
inayotawala katika masomo yetu ya leo ni vita kati wema na ubaya, uongo na
ukweli. Sisi pia tuna vita kati ya wema na ubaya mioyoni mwetu, lakini mara
nyingi tunapoteza muda mwingi kuwahahukumu wengine kuliko sisi wenyewe. Yesu
anatuambia leo kwamba yeye ni mwanga wa ulimwengu, na hatuwezi kuwa katika giza
kama tutamfuata yeye.
Mwishoni mwa injili ya leo, Yesu anakutana tena na Mafarisayo.
Anawapa changamoto kwa kuongea ukweli kuhusu muunganiko wake na Baba yake na
kuhusu nguvu na mamlaka aliyo nayo na utume anao paswa kufanya kwa muunganiko
huu. Mafarisayo wanajaribu kumpa changamoto lakini Yesu anaamua kuongea ukweli
kabisa tena kwa lugha iliyo nyooka kabisa bila kutumia mafumbo. Hakuna nguvu ambayo
ilioweza kumshambulia Yesu iwe ya mafarisayo au ya mtu yeyote kabla ya “saa
yake takatifu haijaja”.
Katika Injili ya Yohane, saa hii takatifu sio saa ya aibu na
kukosa neema kwa Yesu, bali ni saa ya ushindi wake wa kweli juu ya dhambi na
mauti. Katika hali ya kiulimwengu tunajua kuwa siku yake ya kukamatwa, na
kusulubiwa na kutundikwa msalabani ni muda wa woga na hofu. Inaonekana kana
kwamba mafarisayo walishinda na Yesu kupoteza. Lakini katika mtazamo wa
Kimungu, ambao ndio mtazamo wa kweli, Yesu alitukuka kwa utakatifu. Ni wazi,
Kwamba Mungu aliruhusu hali hii ya Mafariso kuwa chombo cha Yesu kujipatia
utukufu kwa njia ya mateso katika wasaa wa Yesu. Katika hali ya Kimungu, wasaa
wake hauwi muda wa kushindwa, bali, unakuwa muda wa ushindi mkubwa.
Muda sio mrefu tutaingia katika utukufu wa juma kuu, na kuona tena
kwamba Baba anaruhusu Yesu aingie katika mateso makali yasio elezeka. Tunaona
changamoto, na tuhuma za kukamatatwa kwake na ushindi wa uongo wa kutokuelewa
wa viongozi wa Wayahudi. Anza kujiandaa katika kuingia katika wasaa huu wa Yesu
na kungara katika ujasiri wa Imani. Tuangalie zaidi juu ya mwanga ulio ndani
mwetu. Tutazame zaidi mtazama wa umilele zaidi kuliko mtazamo wa nje.
Tusitazame zaidi ni kwa jinsi ghani tunafanya njia za msalaba nyingi zaidi,
bali tujiangalie ni namna ghani tunaweza kujisafisha na kukunguta uchafu ndani
mwetu na kujazwa na Mungu zaidi.
Sala: Bwana, Baba amekutuma wewe kwa utume wa kutukomboa sisi na
kuruhusu wewe uteseke na kufa. Lakini kwa njia ya mateso alinunua ushindi wa
mwisho juu ya kifo na mauti. Nipe Imani niweze kuelewa ukweli huu kwa moyo
wote. Yesu, nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment