
“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Jumatatu, Aprili 21, 2025.
Oktava ya Pasaka
Mdo 2:14,22-32
Zab 16:1-2,5-11
Mt 28:8-15.
KUMWABUDU BWANA MFUFUKA!
Habari kuhusu Yesu mfufuka zinaleta hali
mbili kwa wale wanaosikia kuhusu habari hii hapo kwanza. Moja ni muelekeo wa
kumfuata Yesu mfufuka na nyingine ni muelekeo wa kukataa kuhusu Yesu mfufuka.
Wakati wakina Maria na wenzao walikuwa na furaha ya kutangaza habari hii njema
ya ufufuko, viongozi wa Wawayahudi wanahofu na wanaogopa kuhusu kukiri na
kukubali habari hizi. Wakati wakina Maria wanatafuta kila njia na namna ya
kumweleza kila mtu kuhusu habari hii njema ya ufufuko wa Bwana, Viongozi wa
Wayahudi wanatafuta njia ya kuificha habari hii njema isienee kwa kwa watu.
Leo ni siku ya pili katika oktava ya Pasaka.
Ina maana kwamba leo ni Pasaka. Tunasherekea siku ya Pasaka kwa mfululizo wa
siku nane na kuingia katika jumapili ya Huruma ya Mungu. Hivyo siku hizi nane
ni siku ambazo tunapaswa kubaki na kutafakari kwa undani kabisa na kuhisi kama
hawa wanawake watakatifu baada ya kutambua kwamba Yesu hayupo tena kaburini
amefufuka. Tunapaswa kujiachia wenyewe tuingie kwenye mafumbo ya ufufuko.
Tunapaswa kuyaona kama yalivyo. Tunapaswa tutazame zawadi hii, na mshangao wa
hakika wa ufufuko, Yesu ameangamiza matokeo ya dhambi. Aliangamiza kifo
chenyewe.
Wakati hawa wanawake wakitoka kaburini,
maandiko yanatuambia kwamba walikutana na Yesu mfufuka wakiwa njiani. Na
yanasema kwamba walimuona Yesu, na walimkaribia na kuishika miguu yake, na
kumwabudu”. Hili sio tendo dogo la kuabudu na upendo. Kitendo hichi cha
kumtukuza na kumwabudu Yesu kinaonesha kwamba hawaku muamini tu, bali
walimwabudu. Tunapaswa kufanya hivyo, kama wao.
Tutumie muda huu wa Oktava ya Pasaka na
kutafakari juu ya ufufuko na kuwa na muda juu ya unyenyekevu wa kumwabudu Yesu.
Tujiachie wenyewe tuje mbele ya Yesu uso kwa uso, na kumwacha yeye mwenyewe
abadilishe maisha yako.
Sala: Bwana, nina amini. Nina amini kwamba
umefufuka kwa ushindi juu ya dhambi. Ninakuomba unisadie kuelewa na kuhisi hali
hii ya utukufu wa ajabu katika maisha yangu. Ninakuabudu kwa upendo usio
pimika, Bwana mpendwa. Nisaidie nikuabudu wewe kwa hali yangu yote. Yesu, nakuamini
wewe. Amina.
Copyright
©2013-2025 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment