
“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya kwaresima
Jumamosi, Aprili 12, 2025,
Juma la 5 la Kwaresima
Ez 37: 21-28;
Yer 31: 10-13;
Yn 11: 45-56
KUJITAZAMA KIDOGO NA KUMTAZAMA YESU ZAIDI!
Katika Injili ya leo tunaona jinsi Kayafa kuhani mkuu anavyo
fikiri. Maneno yake yanavutia katika hali kwamba ni ya huzuni lakini yanatoa
unabii kwa wakati mmoja. Walitamani na wanaanza kupanga yeye na makuhani
wengine pamoja na Mafarisayo jinsi ya kumkamata Yesu na kumuua. Lakini
kinachotupa kitu ni jinsi ya msukumo wa Kayafa na wengine.
Yesu alikuwa akipata umaarufu na walikuwa wakiogopa umaarufu wake
utachochoea vitu kati ya Warumi. Na walikuwa na wivu kwamba Yesu amewavutia
watu wengi sana. Na Kayafa anatoa mantiki iliojificha kwamba inapaswa mtu mmoja
afe kwa ajili ya watu kuliko taifa zima liangamie. Kwa maneno mengine alifikiri
kwamba kwasababu Yesu anapata umaarufu sana na kwasababu watu wengine walikuwa
wakimsikiliza Yesu zaidi kuliko wao makuhani na mafariyo, ni kwamba “ni vizuri
kuliondoa tatizo” ili mambo yaweze kuendelea kama yalivyo zoea.
Hili linafunua ukweli kwamba Mafariyo walikuwa wakijali zaidi nafsi
zao na umaarufu wao kuliko ukweli. Kama Mafarisayo na Makuhani walikuwa
wanapenda ukweli, wangeona pia utukufu na mamlaka aliokuwa nayo na kumwamini
yeye na kumfuata. Lakini hawakuweza kuacha majivuno yao na kukubali ukweli na
kumfuata mtu mwingine badala ya nafsi zao. Hawakuweza kuachia mamlaka yao.
Hali hii pia tunaiona katika maisha yetu ya kila siku. Mara nyingi
tunataka sisi tuwe kitovu cha kuangaliwa. Na mara nyingi tunavyo muona mtu
mwingine akifanya vizuri au akipokea sifa tunapatwa na wivu mbaya. Na wivu wetu
unageuka na kuwa chuki. Tuna enda mbali na Yesu pia. Tujaribu kufikiria muda
tuliokuwa tukifanya kama Kayafa. Na tunapo ingia katika wiki kuu, tuelekeze
macho yetu kwa Yesu kuliko kwa nafsi zetu. Tujikute sisi wenyewe chini ya
mslaba wake siku ya Ijumaa kuu kwa mapendo na ujasiri, tukisimama karibu na
tukimpenda katika njia zetu zote za maisha.
Sala: Bwana, ninaomba nikufuata wewe katika wiki kuu inayokuja.
Ninakuomba niwe na upendo wa kukupenda wewe hata katika kukataliwa kwako na
uchungu. Ninaomba unisaidie nitupilie mbali wivu na chuki na kukuona wewe
katika mateso ya wengine na katika furaha yao. Yesu, nakuamini wewe. Amina
Amina!
ReplyDelete