“MBEGU ZA UZIMA”
Jumapili, April 16, 2023
Dominika ya Pasaka (Dominika ya 2 ya Pasaka)
Acts 5: 12-16;
Ps 118: 2-4, 13-15;
Ufu: 1:9-19
Jn 20: 19-31
HURUMA YA MUNGU ISIYO NA KIKOMO!
"Hakuna mtu atakayetengwa na huruma ya
Mungu; kila mtu anajua njia ya kuipata huruma hiyo na Kanisa ni nyumba
inayowakaribisha wote na hakuna anayekataliwa. Milango yake inabakia wazi, ili
wote wanaoguswa na huruma waweze kupata toshelezo la msamaha. Dhambi inavyokuwa
kubwa, vivyo hivyo upendo unapaswa Kuwa mkubwa ule ambao unatolewa na Kanisa
kwa wale wote wanaoongoka... Kwa sababu hii, nimeamua kuitisha Jubilei ya hali
ya pekee ambayo ni kuwa na huruma ya Mungu katika kiini chake. Unapaswa uwe
mwaka mtakatifu wa Huruma. Twahitaji kuuishi mwaka huu katika mwanga wa maneno
ya Bwana: "Kuwa na huruma, kama tu Baba yako alivyo na huruma. (Rej. Lk
6:36)." Haya yalikuwa ni maneno ya Papa Francis alipoutangaza mwaka 2016
kuwa ni "Mwaka Mtakatifu wa Huruma."
Leo katika Dominika ya Huruma ya Mungu,
tunakumbushwa juu ya huruma ya Mungu isiyo na kikomo. Injili Leo inaonyesha
mamlaka ya Yesu pale anapowapa mitume, Roho Mtakatifu, ambaye atakayetoa
msamaha wa dhambi.
"Mungu hachoki kamwe kutusamehe; sisi
ndiyo tunaochoka kuitafuta huruma yake. Yesu Kristo, aliyetuagiza tusameheane
"saba mara sabini" (Mt 18:22) ametupa mfano wake yeye mwenyewe:
ametusamehe saba mara sabini... kwa upole usiyotuacha tuaibike, lakini daima
wenye uwezo wa kuturudishia furaha yetu, anatuwezesha kuinua vichwa vyetu na
kuanza upya. Basi sisi tusiukimbie ufufuko wa Yesu, kamwe tusikate tamaa, hata
litokee jambo gani. Maisha yake yawe mfano unaoangazia zaidi ya kitu chochote,
unaotusukuma kwenda mbele!" (Furaha ya Injili, 3)
Sala: Bwana, Nisaidie kamwe nisiwe mbali
nawe, badala yake niiamini huruma yako. Amina.
Copyright
©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment