
“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumatatu, Aprili 14, 2025
Juma Kuu
Isa 42: 1-7;
Zab 27: 1-3, 13-14;
Yn 12: 1-11.
HARUFU NZURI YA UPENDO!
Upendo haujui mipaka. Leo, Maria anafanya
kitu ambacho ni upendo pekee waweza kufanya. Alichukua kitu cha thamani kubwa
kabisa alichokuwa nacho, alichukuwa mafuta na kumpaka Yesu miguu. Kitendo cha
Maria kilisukumwa na kitu kimoja tu, tena kimoja tu, Upendo wake kwa Yesu na
shukrani kwa huruma ya Mungu. Ilikuwa pia muhimu tena kwamba, Maria alimpangusa
Yesu miguu kwa nywele zake, wakati nywele zuri zilizo wekwa vizuri huonyesha
utu wa mwanamke kipindi hicho.
Kawaida mwanamke alijisikia fahari kwa nywele
zake, ambazo zilichukuliwa kama kivutio, na kama mmoja nywele zake hazikuwa
vizuri au kuharibika basi alionekana kama asiye na bahati, au anakosa thamani.
Kwakutumia nywele zake kupangusa miguu ya Yesu, Maria alionyesha hali yake ya
kujishusha na utayari wake wa kumtumikia Kristo. Maria ni mkarimu na ni mfano
wa mfuasi mwema. Anafanya kitu ambacho Yesu angefanya baadae……kuwaosha miguu
wafuasi wake.
Yesu hakuwa mbinafsi kwa upendo wake kwetu
sisi. Kwa kukubali kupakwa mafuta na Maria Yesu anatukumbusha kitu ambacho
tunapaswa kutenda. Tunapaswa kumwabudu, kumheshimu na kumfanya kuwa kiini cha
maisha yetu. Tunapaswa kunyenyekea mbele zake na kumtumikia. Si kwasababu yeye
anataka tufanye vile tu, bali sisi tunapaswa tufanya vile. Kumheshimu kwa
unyenyekevu na upendo ndicho tunacho hitaji kufanya kwasababu ya utakatifu wetu
na furaha yetu. Yesu alitambua hili, hivyo anamsifu Maria kwa upendo huu. Kitendo
hichi kinatukumbusha sisi pia kufanya vile vile. Kinataka tumtazame Yesu na
kumfanya kiini cha kumtukuza na Upendo. Inatualika kuweka kila kazi yetu kwa
Yesu (ambayo inawakilishwa na yale Marahamu, mshahara wa siku 300). Hakuna kitu
ambacho ni cha gharama sana kwa Yesu. Hakuna chenye thamani kubwa kama
Kumwabudu Yesu.
Injili inaeleza kwamba, nyumba yote ilijazwa
harufu nzuri ya marashi aliopakwa Yesu. Alichofanya Maria kinaleta harufu nzuri
ya furaha kila mahali, ni kama siku chache zijazo tutakapo muona Yesu
akituonesha upendo wake wa hali ya juu kwa kutoa kilicho chema kabisa
alichokuwa nacho, ambacho ni kutoa damu yake kwaajili yetu na kutupa Roho wake
Mtakatifu. Tunapata mfano wa upendo ndani ya Maria na ndani ya Yesu, tuombe pia
maisha yetu yatoe harufu nzuri ya upendo wa Yesu.
Sala: Bwana, ninaomba nifuate mfano wa huyu
mwanamke mtakatifu, maria. Bwana mpendwa, hakuna kitu kwenye maisha chenye
thamani kama wewe na majitoleo yangu kwako. Ninaomba unitue kwako Ee Yesu,
ninyenyekeshe mbele ya utukufu wako nisaidie niweze kupenda na kukuabudu kwa
moyo wangu wote. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
Copyright
©2013-2025 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment