
“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Alhamisi, Aprili 10, 2025.
Juma la 5 la Kwaresima
Mwa17: 3-9;
Zab 104: 4-9;
Yn 8: 51-59.
AGANO LA UPENDO!
Lirtujia na Neno la Mungu linatualika sisi
kukumbuka Agano la Mungu nasi kwa njia ya Yesu. Somo la kwanza linaonesha
ukarimu wa Mungu akifanya Agano na Abram, na kuingia katika historia ya
Mwanadamu. Ukuu wa Abramu umejikita katika Imani yake na utii kwa Mungu. Bila
hata kujua Abram ana anza safari kwenda nchi asio ifahamu. Kwa kumuita Abram
Mungu alibadilisha maisha yake yote. Kwa mara ya kwanza katika historia ya
Mwanadamu Mungu anabadilisha jina la mtu. Abram anaitwa Abrahamu. Ikiwa na
maana kwamba Mungu anauwezo wa maisha yetu yote ya sasa na ya baadae. Agano la
Mungu halifungwi tu kwa Abrahamu na familia yake tu. Kama mto unaotiririka
daima limejaa ukarimu. Anacho taka Mungu kutoka kwetu ni kudumisha Agano hili
daima.
Katika somo la Injili, Yesu anawaita watu
waheshimu Agano la Mungu. Kama watalishika Agano hili hawataona mauti. Kwani
kifo ni matokeo ya dhambi. Kwasababu ya kutotii Mwanadamu alipoteza heri
machoni pa Mungu lakini Agano la Mungu kwa njia ya Yesu ni kuirudisha tena ile
neema iliyopotea.
Sala: Bwana, ninakuomba Moyo wako uweze
kuchuja makosa yangu yote na kuruhusu mbegu ya ukweli kumea ndani ya akili na
moyo wangu. Mungu wa Agano, tusaidie pia sisi tuweze kuwa waaminifu kwa maagano
yetu nawe. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment