
“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya Kwaresima
Machi 29, 2025.
------------------------------------------------
JUMAMOSI, JUMA LA 3 LA
KWARESIMA
Somo la 1: Hos 6:1-6
Mungu anawaambia watu wake wamrudie: “Ni upendo anahitaji sio sadaka, na elimu
ya Mungu kuliko sadaka ya kuteketezwa”.
Wimbo wa katikati:
Zab51: 3-4, 18-21 Ninachohitaji ni upendo sio sadaka.
Injili: Lk 18: 9-14 Luka
analinganisha haki ya kujitakia ya Mafarisayo na unyenyekevu wa watu
waliomfuata Yesu, waliojitambua kuwa ni wadhambi wanaohitaji huruma.
------------------------------------------------
SALA NI KUJIONA MWENYEWE
KWA NJIA YA JICHO LA MUNGU
Mungu anaenda kwa watu
aliowachangua, mpendwa Efraim na Yuda, ambao wapo mbali na Mungu, waliokamatwa
katika matatizo yao. Mungu alitaka watambue kwamba ingawaje ndiye yeye
aliyewapa adhabu lakini pia ni yeye atakaye ponya magonjwa yao. Kama
tutajitahidi kwenda kwa Bwana atakuja kwetu upesi kama vile mvua inavyo
inyeshea ardhi. Lakini Mungu anaifahamu Efraim na Yuda na sisi pia. Fadhila
yetu ni kama tone la umande ambalo hupotea. Uaminifu wetu ni mdogo na hafifu.
Mfano wa Yesu wa
Mafariyo na watoza ushuru unaelekezwa kwao wote ambao hujiamini wenyewe kama
watakatifu na kuona wengine wadhambi. Watu wawili walioenda hekaluni kusali.
Mmoja anasimama mbele ya Mungu bila kujinyenyekesha na kusali kwa nguvu, huku
akiwalaumu mwengine na kujiinua na kujitakia haki. Mwingine ni Mtoza ushuru
anaye kakaa nyuma na kujiona mdhambi na kumwambia Mungu “unihurumie mimi kwani
ni mdhambi”.
Je, tunasalije? Huwa
tunamwambia Mungu ni kwa jinsi ghani tulivyowazuri na kutaka Mungu atusifie? Au
je huwa tunaona uhusiano wetu wa kweli na Mungu? Kama ukweli wa Mungu ukitujaza
sisi lazima tutajazwa na ukweli kuhusu dhambi zetu na ukosefu wetu wa mapendo.
Sisi ni wadhambi na tunahitaji huruma ya Yesu hata katika kusali tunahitaji
Roho atuongoze ili tuweze kumwomba Mungu vizuri.
Leo hii tunakazana kwa
akili zetu wenyewe. Na tunajiona wenyewe kwamba kitu fulani ni hakika. Mungu
anatuaona sisi kama tulivyo. Anaona mambo yote mazuri na yale ambayo tunapaswa
kukazana kuyapigania. Anaona yale mambo ambayo yapo ndani kabisa mwa mioyo yetu,
ambayo ni upofu katika maisha yetu. Mungu anatupenda kama tulivyo. Hivyo
tujiangalie sisi wenyewe kwa jicho la mkombozi wetu. Tukijiona wenyewe kama
Mungu anavyofanya tutakuwa tayari kupokea huruma yake na neema.
Sala: Bwana, upendo wako
unaniambia kwamba niungame na kurudi kwako. Kujitakia kwangu haki kunanifunga
mimi nishindwe kuona makosa yangu. Ninaomba neema yako inisaidie mimi niweze
kuona neema yako kama wewe unavyo niona mimi. Amina
No comments:
Post a Comment