MASOMO YA MISA, MACHI 29, 2025
JUMAMOSI , JUMA LA 3 LA KWARESIMA
SOMO 1
Hos. 5:15-6:6
Bwana asema: Katika taabu yao watanitafuta kwa
bidii:
Njoni, tumrudie Bwana; maana yeye amerarua, na
yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga jeraha zetu. Baada ya siku
mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tuataishi mbele zake. Nasi na
tujue, naam, tukaendelee kumjua Bwana; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi;
naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyeshayo nchi.
Ee Efraimu, nikutendee nini? Ee Yuda, nikutendee
nini? Kwa maana fadhili zenu ni kama wingu la asubuhi na kama umande utowekao
mapema. Kwa sababu hiyo nimewakata-kata kwa vinya vya manabii; nimewaua kwa
maneno ya kinywa change na hukumu yangu itatokea kama mwanga. Maana nataka
fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 51:1-2, 16-19 (K) Hos. 6:6
(K) Ninavyotaka ni fadhili, si sadaka.
Ee Mungu, unirehemu,
Sawasawa na fadhili zako.
Kiasi cha wingi wa rehema zako,
Uyafute makosa yangu.
Unioshe kabisa na uovu wangu,
Unitakase dhambi zangu. (K)
Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa,
Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.
Dhabihu za MUngu ni roho iliyovunjika;
Moyo uliovunjika na kupondeka,
Ee Mungu, hutaudharau. (K)
Uitendee mema Sayuni kwa radhi yako,
Uzijenge kuta za Yerusalemu.
Ndipo utakapopendezwa na dhabihu za haki,
Na sadaka za kuteketezwa, na kafara. (K)
SHANGILIO
Eze. 18:3
Tupilieni mbali nanyi makosa yenu yote
mliyoyakosa yote, asema Bwana, jifanyieni moy mpya na roho mpya.
INJILI
Lk. 18:9-14
Yesu aliwaambia mfano huu watu waliojikinai ya
kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Watu wawili walipanda kwenda
hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama
akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu
wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi
nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mpato yangu yote. Lakini yule
mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni,
bali alijipiga-piga kifua akisema, ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.
Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule;
kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright ©
2025, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment