
“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya kwaresima
Ijumaa, Machi 14, 2025
Juma la 1 la Kwaresima
Eze 18:21-28;
Zab 130: 1-8;
Mt 5:20-26.
KUWA MWEMA!
Leo, Nabii Ezekieli anaweka mbele yetu
matarajio ya Mungu kwetu sisi. Anatoa sura ya Mungu akiwa amejawa na huruma kwa
wale wote ambao hutubu dhambi zao. Hata hivyo anamuonesha Mungu akiwa hakimu wa
haki aliye mwema asiye pendezwa na mabaya. Mungu hataki mtu aliye katika pande
mbili (anayechanganya mema na mabaya kwa wakati mmoja), yeye anatazama kila
mmoja wetu katika nafsi nzima.
Katika Injili Yesu anaongelea kuhusu Ufalme
wa Mbinguni. Kuingia katika Ufalme wa mbinguni unapaswa kuwa lengo la Maisha
yetu. Ni mara nyingi tunashindwa kuliona hili katika maisha. Tunashindwa
kufungua macho yetu kuelekea Mbinguni kama lengo letu la kwanza la kuwa hapa
duniani. Ni rahisi kunaswa na kuridhika na hali za kila siku kama viburudisho,
pesa, mafanikio, na mengineyo.
Yesu anatupa njia ya pekee ya kufuata katika
ujumbe huu wa Injili, jinsi ya kupata lengo la maisha-ufalme wa Mbinguni. Njia
anayo ionesha ni haki. Haki maana yake ni kuwa mwaminifu, sio mdanganyifu.
Mafarisayo walijifanya kwa kujionesha kuwa walikuwa watakatifu na wafuasi
wazuri wa mapenzi ya Mungu. Lakini hawakuwa wazuri katika hilo. Wanaweza kuwa
wazuri katika hali ya kutenda na huenda wanaweza kuwa wamewavutia watu, lakini
hawakuweza kumdanganya Yesu. Yesu aliweza kuona udanganyifu wao na kujificha
kwao kusiko kwakweli na akaona kile kilicho jificha. Yesu aliweza kuona haki
yao ni kwa ajili tu ya kujionesha wenyewe kwa watu.
Kama tunataka kufanya Mbingu kuwa lengo letu,
tunapaswa kujitahidi kuwa watakatifu. Na waaminifu. Tunapaswa kumtafuta Kristo
katika hali ya kweli na uaminifu katika vitu vidogo vya maisha. Tunapaswa
kuacha uaminifu huo uweze kungaa kwa kuonesha katika kweli kile kilichopo
katika hali ya ndani. Kuwa wenye haki katika hali ya kweli, ni kwamba
tunamtafuta Yesu katika hali ya haki na kumfanya Mungu kuwa lengo la maisha
yetu.
Sala: Bwana, naomba unifanye mwenye haki.
Nisaidie niweze kuwa mwaminifu kwa yote ninayofanya na yote ninayo tafuta
katika maisha. Nisaidie mimi nikupende wewe kila wakati na siku zote. Yesu, nakuamini
wewe. Amina
No comments:
Post a Comment