
“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumamosi, Machi 22, 2025,
Juma la 2 la Kwaresima
Mika 7:14-15,18-20;
Zab 103;1-4, 9-12;
Lk 15: 1-3, 11-32
KUMRUDIA MUNGU!
Katika mfano wa Mwana mpotevu tunaona ujasiri
wa huyu Mwana kwa kuchagua kurudi kwa Baba yake. Ni kweli, alitambua udhaifu
wake na akaamua kurudi kwa Baba yake kuomba msamaha na kumuomba amfanye kama
mmoja wa wafanyakazi wake. Alifanikiwa kurudi.! Swali la kujibu “kwanini?”
Ni vyema kusema kwamba huyu mtoto alirudi kwa
Baba yake, kwanza kabisa kwasababu alitambua kutoka moyoni mwake tabia ya Baba
yake. Baba alikuwa Baba mwema. Alionyesha kujali na kuwa na upendo kwa mtoto
daima katika maisha yake. Ingawaje mtoto alimkimbia Baba yake, haikubadilisha
ukweli kwamba yeye alitambua kuwa Baba yake alikuwa mtu mwema na kwamba
anampenda. Pengine hakutambua ni kwa jinsi ghani, hadi alipo tambua mwenyewe.
Ni wazi kwamba ni kwasababu ya utambuzi huu kutoka moyoni mwake unaompa ujasiri
wa kurudi kwa Baba kwa matumaini ya upendo wa Baba yake.
Hili linafunua kuwa, upendo wa kweli unafanya
kazi. Daima unafanya kazi. Hata kama mtu akikataa upendo mtakatifu tunaompa,
lazima daima una ongeza kitu katika maisha yao. Upendo wa kweli usio na
masharti ni vigumu kuukataa na kuutupilia mbali. Mwana mpotevu alitambua hili,
na sisi pia tunapaswa kuwa hivyo. Huu ndio upendo alionao Baba yetu wa Mbinguni
kwa kila mtu. Yeye sio Mungu mkali na mgumu. Ni Mungu anayependa kuturudisha kwake
na kutupatanisha naye. Anafurahi tunapo mrudia na kuomba mahitaji yetu kwake.
Ingawaje tuna wasi wasi, yeye hana wasi wasi kwa upendo wake, daima anatusubiri
sisi, na sisi wenyewe kutoka ndani kabisa tunatambua hilo.
Kwaresima ni kipindi kizuri sana kwa
sakramenti ya kitubio. Na sakramenti hiyo ndio ujumbe wote katika mfano huu. Ni
mfano wa sisi kwenda kwa Baba yetu na dhambi zetu na atatupokea kwa huruma.
Inaweza kuogopesha na kuwa na wasi wasi kwenda kwenye sakramenti ya kitubio,
lakini tukiingia katika sakramenti hiyo kwa uaminifu na katika kweli, tunaona
furaha tunayopata na Amani kuu. Tunajisikia Amani na kuacha mizigo iliyo
tuelemea rohoni. Mungu, anatukimbilia, na kunyanyua mizigo yetu na kuitupa
nyuma yetu. Usikubali kipindi hichi cha kwaresima kipite bila kuungama! Hakuna
na tena, wala hakuna sehemu nyingine waweza kupata furaha hii ya kuunganika na
Mungu katika kweli. Usijioneee huruma kwa kujibembeleza kwamba nitamweleza tu
Mungu mwenyewe nikiwa chumbani kwangu. Nenda kaungame katika hali ya uaminifu
na kweli kadiri ya Imani yetu. Mungu anakusubiri. Usikubali kubaki katika
gereza la dhambi. Fanya uamuzi kama Mwana mpotevu.
Sala: Baba, nilienda kinyume na wewe na
kufuata njia zangu mwenyewe. Sasa ni muda wa kurudi kwako katika hali ya uwazi
na uaminifu wa moyo. Ninaomba unipe ujasiri huo ili niweze kukumbatia
sakaramenti ya kitubio. Yesu nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment