“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumatano, Machi 12, 2025
Juma la 1 la Mwaka
(siku ya wanawake duniani)
Jon 3:1-10;
Ps 51:3-4,12-13,18-19;
Lk 11:29-32
KUMKUBALI YESU NA UPENDO WAKE!
Katika masomo ya leo tunamwona Yona akipeleka
Neno la Mungu kwa watu wa Ninawi, na anapo anza kuingia katika mji, anaanza
kutangaza kwake kuharibiwa kwa mji huo na watu wanasikia . Mfalme anasikia na
kutangaza kufunga, watu wavae magunia wajipake majivu na kutubu. Mfalme
mwenyewe ana anza kuvaa magunia, kuacha kiti chake cha enzi na kukaa katika
majivu. Hivyo Mungu anawaonea huruma watu wa Ninawi na ana sitisha mpango wa
kuuharibu mji huo. Muujiza huu sio Mungu kuacha kuuanga miza mji wa Ninawi bali
ni namna watu walivyo mgeukia Mungu. Walipokea neno la Mungu na wakaliweka
katika matendo.
Katika Injili, tunaona watu ambao wanahitaji
ishara ya ajabu ili waweze kusikiliza maneno ya Yesu. Yesu anashangazwa na
anawaambia, Malkia wa Sheba alikuja kutoka mbali kumsikia Sulemani na Ninawi
walitubu baada ya kumsikia Yona, wao wapo na mtu mkubwa zaidi kuliko Yona na
Sulemani lakini wanashindwa kumtambua. Wapo na mwana wa Mungu lakini kwasababu
ya mioyo yao migumu wanashindwa kumtambua Yesu nakuongoka.
Watu wakipindi cha Yesu walibarikiwa kwa
kusikia neno la Mkombozi wa Ulimwengu. Je, na sisi pia?! Tuna Injili,
mafundisho ya Kanisa, ushahidi wa Watakatifu wengi, uchungaji wa Baba
Mtakatifu, Sakramenti na mengine mengi. tuna njia mbali mbali za kupata Injili
katika Ulimwengu wa Teknologia lakini ni ajabu tunaweza kushindwa kusikia sauti
ya Yesu. Tutafakari sisi wenyewe jinsi tunavyo itikia ujumbe wa Yesu. Anaongea
na sisi mara nyingi kwa nguvu mbali mbali lakini tunashindwa kumsikia.
Kushindwa kusikiliza, inapelekea tunashindwa kutubu.
Sala: Bwana, unaongea nami kwa njia mbali
mbali. Unahubiri kwa njia ya Neno lako, Kanisa lako na katika maisha yangu ya
sala. Ninakupenda wewe, Bwana wangu mpendwa, ninatubu dhambi zangu. Yesu
nakuamini wewe. Amina.
Copyright
©2013-2025 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment