
KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Ijumaa, Machi 28, 2025,
Juma la 3 la Kwaresima
Hos 14:2-10;
Zab 81:6-11,14,17;
Mk 12:28-34
CHAGUA KUMPENDA MUNGU!
Mwandishi alimuuliza Yesu, “ni amri ipi iliyokuu?” na Yesu akajibu
ni “Upendo”. Upendo tunao ufahamu na kuhisi katika maisha ni “hali ya
kujisikia/kuhisi kutoka ndani mwetu”; hisia, au hali ya kujisikia tunayo
ilinganisha na vitu tulivyopokea au kutamani. Katika hali fulani vitu na watu
huongoza upendo wetu.
Lakini, anachosema Yesu kuhusu “upendo” ni kitu kingine tofauti.
Huu ni upendo ambao tunaweza kuumudu, tunao amua kuutoa. Mungu haitaji upendo
wetu ili yeye aweze kuishi. Lakini ameamua kutupatia maisha. Hii si kwasababu
anatuhitaji sisi, bali kwasababu anapenda kuutoa. Hii ndio maana ya upendo wa
Mungu usio na masharti. Anachotaka Mungu kutoka kwetu ni kuchagua kumpenda yeye
kama yeye alivyo chagua kutupenda sisi. Na tunapo fanya hivyo tunapokea upendo
wake zaidi, kwani tunabaki katika upendo wake. Kwahiyo, leo tuchague kumpenda
Mungu kwa akili zetu zote, na hapo hatutakuwa mbali na ufalme wake.
Hatua ya kwanza katika kumpenda Mungu ni kutaka kumfahamu. Hii ina
maana tunapaswa kutafuta jinsi ya kumfahamu, na kutaka kumuelewa na kumwamini
Mungu na yote yaliyo funuliwa kwetu kuhusu yeye. Ina maana tumeamua kujikita
katika kuingia kufahamu mafumbo ya maisha ya Mungu, hasa kwa njia ya Maandiko
Matakatifu na kwa njia ya ufunuo wa mafundisho ya Kanisa katika historia ya
Kanisa. Pili, tunaingia katika undani kwa kufuata njia zake. Jambo hili la
uhuru kamili linapaswa kufuata akili yetu kuhusu yeye na kuwa kitendo cha Imani
kwake. Tatu, tunapo ingia katika kutaka kuyaelewa mafumbo ya maisha ya Kimungu
na kuchagua kumwamini na yote aliyo tufunulia, tutaona maisha yetu
yatabadilika. Njia maalumu itakayo badilika ni kwamba tuta tamani kuwa na Mungu
na kufanya mapenzi yake katika maisha yetu, tuta tamani kumtafuta zaidi,
tutapata furaha kwa kumfuata na tuta tambua kuwa upendo wa roho yetu kama
wanadamu utazama katika upendo wake na katika njia yake. Tafakari ni mara ngapi
umetamani kumfahamu Yesu na kutaka kufahamu yote aliyo tufunulia.
Sala: Bwana, ninaomba niwe mwaminifu katika kujikita kwangu ili
niweze kukufahamu zaidi na kufahamu ukweli wa utukufu wa maisha yako.
Ninakushukuru kwa yote ulionifunulia mimi na ninajitolea maisha yangu, leo,
katika harakati za kufahamu maisha yako na ufunuo wako. Yesu nakuamini wewe.
Amina.
No comments:
Post a Comment