“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba 4, 2024.
------------------------------------------------
JUMATANO, JUMA LA 1 LA MAJILIO
Somo la 1: Isa 25:6-10 Isaya anaona maono kuhusu furaha ya milele mbinguni wakati njaa ya kila mwanadamu itakapo shibishwa, na Bwana Mungu atafuta machozi yote kutoka katika kila uso.
Wimbo wa Katikati: Zab 22:1-6 Bwana ndiye mchungaji wetu. Katika malisho ya majani mabichi, hutupa pumziko.
Injili: Mt 15:29-37 Yesu anawaponya viwete na wagonjwa wengi, anawalisha umati kwa mikate na samaki, kimiujiza.
------------------------------------------------
NJAA YA KUMPATA MUNGU
Injili inaelezea kuhusu kuponjwa kwa viwete, wenye magonjwa, vipofu na bubu. Miujiza ya namna hii ilivutia watu wengi. Muujiza wa kulishwa kwa watu wengi ulikuwa ni utabiri wa karamu ya Ekaristi ambayo ilikuwa inakuja.
Tunasomo kwamba umati huu mkubwa ulikuwa na Yesu kwa siku tatu katika jangwa. Chakula kilikuwa kidogo na watu karibia wote wame karibia kumaliza kila kitu walichokuwa nacho. Wakina mama walikuwa na hofu juu ya watoto wao. Waliokuwa wadogo walikuwa wamechoka kwa kukaa siku tatu. Wanaume nao walijisikia ni lazima kutafuta kitu sasa kwa ajili ya familia zao. Yesu alisukumwa na huruma. Mikate saba na samaki wachache aliwaongeza kimuujiza na kushibisha watu wote hadi kusaza na kubakiza.
Njaa ya mwanadamu ya kumtafuta Mungu na njaa ya mwanadamu ya kutafuta chakula na kunywa vinaweza kuwa ishara ya ndani kabisa ya njaa zote. Mfano wa njaa ya chakula sio. Kula chakula sana au kunywa sana inaweza kumfanya mmoja kuwa mgonjwa au kuzidisha uzito na hivyo kuanza kupunguza kwakufanya mazoezi. Lakini katika maisha ya kutumia chakula cha kiroho, Ekaristi takatifu ambacho humfanya mtu kuwa mpya, haina kupunguza uzito kuhusu mambo ya kiroho wala mambo ya mbinguni.
Ni katika mwanga Yesu anatambulisha muujiza kwa neno lake. “Moyo wangu umejaa huruma kwa ajili ya mkutano…sitaki kuwaacha waende bila kula, wasije wakazimia njiani”. Siku hiyo aliwalisha kwa mkate na samaki. Na sasa anatulisha kwa mkate na divai, mwili na damu yake. Anatoa ukamilifu wa kile kinacho onekana katika muujiza huu, Ekaristi, na hivyo anatupatia karamu ya mbinguni ambayo imeshasemwa na Isaya. Kupokea komunyo takatifu inatusaidia sisi kukutana na Yesu kama Mkombozi. Muujiza huu unatualika kuendeleza kuzidisha kuwagawia maskini vile ambavyo Mungu anatuzidishia na kuwaruhsu washiriki katika yale tulio nayo, kama wanadamu, kama Isaya anavyosema “ni karamu ya chakula cha utajiri na divai nzuri”.
Sala: Bwana, ninakushukuru kwa huruma yako na zawadi ya Ekaristi, ambapo kwa njia yake unatuliza njaa yetu na hivyo kutushirikisha chakula cha mbinguni. Ninakuomba niweze kuwa makini katika kukupokea katika Ekaristi. Amina
Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment