“ASALI ITOKAYO MWAMANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatatu, Novemba 18, 2024,
Juma la 33 la Mwaka wa Kanisa
Ufu:1:1-4, 2:1-5;
Zab 1:1-4, 6;
Lk:18:35-43
“WATAKA NIKUFANYIE NINI?”
Inavutia kumsikiliza Yesu akimuuliza mtu anataka nini. Tunaweza kufikiri kuwa ni kawaida, lakini kwanini Yesu anauliza mambo yanayoeleweka? Huenda ikawa nikwasabababu mbili zifuatazo: Kwanza, kuongeza imani na kufanya mtu akiri hiyo Imani, au, Pili kumsaidia mtu husika agundue kile alichokiomba kwa Yesu. Swali hili linaweza kuwa na manufaa kwetu sisi wafuasi wake. Ukweli ni kwamba, baadhi yetu, pengine hatupendi kuponywa, tunahitaji tu Baraka na sala,na pengine hatuhitaji uponyaji wa kweli. Tunafurahia hali yetu ilivyo ili tuendelee kupata msaada ambao tunaupata kwa sababu ya kupata madhara ya ugonjwa fulani au matatizo fulani. Sisi tunapaswa kuwa kama yule kipofu ambaye hakujificha, na wala hakujali ni namna gani anaweza kuonekana mbele ya watu wengine kwasababu ya ugonjwa wake na bila kuogopa anamuita Yesu kwa imani. Ni jinsi gani mambo yetu yangekuwa tofauti kama wewe na mimi tungeboresha mahusiano yetu na Mungu na kumwita kwa imani?
Sala: Ee Bwana, ninajongea kwako kwa imani na matumaini. Nikirimie mtazamo mpya na hali mpya. Amina.
Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment