Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

UAMINIFU WA MUNGU!



“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Alhamisi, Novemba 28, 2024, 
Juma la 34 la Mwaka wa Kanisa

Ufu 18:1-2, 21-23; 19:1-3, 9; 
Zab 99:2-5; 
Lk 21:20-28


UAMINIFU WA MUNGU!


Liturjia ya leo inatukumbusha uwepo wa Mungu katika maisha yetu ya kila siku. Inaongelea kuhusu siku ya hukumu, siku ya ujio wa pili wa Kristo atakaye kuja kuhukumu ulimwengu. Siku hii ni siku ya utukufu kwa waaminifu wote wa Kristo na wafuasi wake.

Leo katika Injili Yesu anatabiri kuhusu kuharibiwa kwa Yerusalemu na kutakaswa kwa ulimwengu mzima. Yesu haongei yote haya ili kututisha, bali anatualika kila mmoja wetu asimame imara na kujiandaa ili kumpokea yeye Masiha wa ulimwengu. Siku ya hukumu ni siku ya kufurahi na kuimba ALELUYA kwa waaminifu wote wa Mungu, kumuimbIa Mfalme wetu. Waaminifu wataimba nyimbo kwa furaha na sala kumuelekea Mungu na Bwana wetu Yesu Kristo. Wapo pia sasa mbele ya Utatu wakifurahi wakiwa wamejawa na furaha kamili. Sala zao hujibiwa wanapo karibia mbele za Mungu kama moshi wa ubani nyumbani mwa Mungu.

Sala: Bwana, nisadie niweze kuweka mawazo yangu katika vitu vya mbinguni ili niweze kusheherekea ujio wako kwa furaha na shangwe. Amina

Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment