“MBEGU ZA UZIMA”
Tafakari ya kila Jumapili
Novemba 17, 2024,
Dominika ya 33 ya Mwaka
Dan 12: 1-3;
Zab 16: 5, 8-11 (K) 1;
Ebr 10: 11-14, 18;
Mk 13: 24-32.
KRISTO TUMAINI LETU!
Leo ni Jumapili moja kabla ya Jumapili ya mwisho wa mwaka katika mwaka wa Kanisa na leo Liturujia inatualika kufikiria kuhusu hukumu ya mwisho kama utangulizi kabla hatuja sherekea sikukuu ya Kristu Mfalme Jumapili ijayo. “Hakuna usiku na giza unaoweza kukaa tuu bila kuwepo asubuhi”. Katika maisha ya Kanisa, Ulimwengu, watu wake na waume, hakuna hali ambayo ni ngumu na inayofunga hali zote kusiwepo na alama ya tumaini. Somo la kwanza na Injili yanatualika kutambua alama hizi za Ulimwengu mpya utakaozaliwa kwetu baada yakuangushwa kwa utawala wa yule muovu.
Somo kutoka kitabu cha nabii Daniel, kilichoandikwa kipindi cha mateso makubwa ya Waisraeli wakiwa chini ya utawala wa Antiokus wa Syria, kinaeleza kwamba mateso yao yatafikia mwisho wake siku moja na Bwana anawatia moyo wabaki waaminifu ili waweze kunyanyuliwa katika uzima wa milele. Wakati akitoa faraja kwa Wayahudi wa wakati huo, unabii huu pia unakumbusha watu wa kila kizazi kwamba Mungu ni mweza na mtawala wa vyote na atakuja kuleta haki Duniani.
Unabii huo huo unaotolewa katika Injili, wakati Yesu mwenyewe alivyosema kwa uhakika kwamba hukumu ya mwisho ipo na ni hakika sio maneno matupu au kitu chakufikirika tuu. Akizungumza kuhusu majaribu/mateso, akiwa analenga sehemu ya kuharibiwa kabisa kwa hekalu la Yerusalemu na mateso yatakayo andamana nayo-hata hivyo yalitokea miaka 40 baadaye mwaka 70 A.D-anaongelea pia kuhusu siku za mwisho, akiwahakikishia pia wale walio waaminifu, lakini akiwaonya pia wale waovu. Je sisi tupo upande ghani?
Katika kutambulisha ujumbe kutoka barua kwa Waebrania kutoka somo la pili, katika hali nzuri kabisa Kanisa linabadilisha muonekano wa kuogopa “matisho” au picha ya matisho katika siku ya hukumu, kuwa ni siku ya zawadi ya Mungu ya kumtuma Mwana wake. Katika mwanga wa siku ya hukumu, upendo usio na mwisho wa Kristu kuwa mwanadamu ni dhahiri na utaonekana. Kwa kuchukua mzigo wa dhambi zetu yeye mwenyewe, alijitoa mwenyewe asulubiwe kwa ajili yetu, akitubadili kutoka kuwa viumbe vyenye hukumu na kutufanya kuwa watoto wa Baba.
Waisraeli waliwachagua na kuwapaka mafuta Makuhani kwa ajili ya kutolea sadaka kwa ajili kuomba msamaha wa dhambi zao walizotenda mwaka baada ya mwaka. Lakini ni Kristo pekee aliyekuhani mkuu, ambaye ametolea sadaka ya milele, alileta wokovu kwa wanadamu wote. Sisi ni nani hata tupate matunda ya mateso yake? Msalabani, Yesu, akiwa anateseka kwa maumivu makali kutoka kwa watesi wake, alimuomba Baba yake awasamehe maadui wake. Katika msamaha, sio kwamba tunamuomba tu Mungu awasamehe maadui wetu katika siku ya hukumu bali sisi pia tunapata msamaha.
Tumezungukwa na mabaya/mashaka kila upande. Na zaidi sana, tunasumbukia sana wakati ujao tukijiuliza baadaye nitaishi je, tukisahau ukweli ni kwamba tuna nguvu ya kujenga maisha yetu ya baadaye tukiwa tumeegemea kwenye neno la Mungu. Tukiamua, tunaweza tukaishi tukahisi uwepo wa mbinguni kati yetu katika maisha yetu ya kila siku. Tusije tukasubiri vitu vitokee kwetu ila tuitike wito na tufanye vitu vitokee kwa ajili yetu, kila wakati.
Sala: Ee Bwana, kwako kunapatikana msamaha na wokovu, na kwa ajili hiyo, tunakupa sifa na shukrani. Amina.
Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment