Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

NENO LA MUNGU



“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa, Oktoba 4, 2024, 
Juma la 26 la Mwaka wa Kanisa

Ayu 38: 1, 12-21, 40:3-5
Zab 139: 1-3, 7-10, 13-14
Lk 10: 13-16


NENO LA MUNGU


Imekuwa kama fasheni siku hizi mtu kuulizia kuhusu uwepo wa Mungu. Huku wakirejea mateso na maovu yaliopo ulimwengu, kiasi cha kuwafanya watu wengine kuwa vigumu kumtafuta au kuwa karibu na Mungu. Kadiri ya watu wanao jiita wa kisasa, mtu amejifanya mwenyewe kwasababu akili imeshindwa kuoanisha kati ya Mungu anayetupenda na maovu yanayotendeka katika jamii, wanaona ni vizuri kuachilia mbali swala la Mungu au kumkataa. Kitabu cha Ayubu kinajibu baadhi ya maswali juu ya uwepo wa Mungu mwema anayetupenda na uwepo wa maovu ulimwenguni. Ayubu mtu mwaminifu na aliyejikita kwa Mungu anateseka vikali katika mikono ya yule muovu. Marafiki zake wanahitimisha kwamba ni kwasababu ya dhambi zake. Lakini , Ayubu alitambua kwamba alikuwa sahihi, na ndio maana alijaribu kumuuliza Mungu yeye mwenyewe! Katika somo la leo Mungu anamjibu Ayubu! Ingawaje majibu ya Mungu yamejitengeneza katika hali ya maswali, bado Ayubu anafurahia majibu hayo. Ayubu alitaka kuwa na uhakika juu ya sababu ya mateso yake. Kama ni Mungu amependa ateseke, yeye alikuwa tayari. 

Bwana: Bwana, niongoze kwenye Neno lako kwa njia ya Neno wako. Amina


Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment