Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MUNGU WA VITU VIDOGO




“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumamosi, Oktoba 5, 2024, 
Juma la 26 la Mwaka wa Kanisa



Ayu 42: 1-3, 5-6, 12-17 
Zab 118: 66, 71, 75, 91, 125, 130
Lk 10: 17-24


MUNGU WA VITU VIDOGO!


Somo la kwanza leo linatueleza ni kwa jinsi ghani Mungu alivyo zibariki siku za mwisho za Ayubu zaidi hata ya zile za mwanzo. Na Ayubu aliamini kwamba Mungu anaweza kutenda na kutoa vitu vyote kwa mwanadamu na kwamba hakuna lengo lake linalo weza kuzuiwa na kitu chochote au nguvu za muovu. 

Wale sabini wanavyorudi wakielezea ushindi, kuna aina tatu za furaha katika Injili ya leo: 1) Furaha ya huduma 2) Furaha ya ukombozi) 3) Furaha ya mamlaka. Yesu aliwapa nguvu na uwezo wakuponya na kutoa pepo wabaya, na kuhubiri Neno, na hatimaye walishinda. Kila ushindi ni muhimu kwa Yesu, haijalishi ni namna ghani waweza kuonekana machoni petu. Lakini, Wafuasi hawapaswi kufurahi kwasababu pepo wabaya wana watii na kuwatoka watu bali kwasababu majina yao yameandikwa mbinguni. Furaha au ushindi waweza kumfanya mtu kuishia kujivuna. Muujiza mkubwa kuliko wote ni ukombozi wa roho iliyopotea. Furaha yetu haipatikani katika huduma, na wala si katika ukombozi, bali ni katika kujikabidhi kwenye mapenzi ya Baba Yetu wa Mbinguni, kwasababu hii ndio sababu ya huduma na ukombozi. 

Sala: Ee Bwana, tuongoze kwenye njia ya udogo na unyofu wa Moyo. Amina

Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment