Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, OKTOBA 15, 2024




MASOMO YA MISA, OKTOBA 15, 2024
JUMANNE, JUMA LA 28 LA MWAKA 


KUMBUKUMBU YA MT. TERESIA WA AVILA, BIKIRA NA MWALIMU WA KANISA


SOMO 1
Gal 5:1-6 

Katika ungwana huo kristo alituandikia huru kwa hiyo simameni wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa. Tazama mimi Paulo nawambia ninyi ya kwamba mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno. Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye,kwamba ni wajibu wake kutimiza torati yote.Mmetengwa na kristo mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria ; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. Maana sisi kwa roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya Imani.Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno,wala kutotahiriwa , bali Imani itendayo kazi kwa upendo.

Hilo  ndilo neno la Bwana… Tumshukuru Mungu


WIMBO WA KATIKATI
Zab 119:41,43-45,47-48

(K) Ee bwana fadhili zako zinifikie na mimi

Ee bwana fadhili zako zinifikie na mimi
Naam wokovu wako sawasawa na ahadi yako
Nami nitamjibu neno anilaumuye
Kwa maana nalitumainia neno lako (K)

Nami nitaitii milele na milele
Naam milele na milele
Nami nitakwenda panapo nafasi
Kwa kuwa nimejifunza mahusia yako (K)

Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako
Ambayo nimeyapenda
Na mikono yangu nitayainulia
Maagizo yako niliyoyapenda
Nami nitazitafakari amri zako. (K)


SHANGILIO
Zab 119:135

Aleluya ,aleluya,
Umwangazie mtumishi wako uso wako,
Na kunifundisha amri zako.
Aleluya.


INJILI
Lk. 11:37-41

Yesu alipokuwa akinena, Farisayo mmoja alimwita aje kwake ale chakula; akaingia, akaketi chakulani. Farisayo huyo alipomwona, alistaajabu kwa sababu hakunawa kabla ya chakula. Bwana akamwambia, Ninyi Mafarisayo mwasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani yenu mmejaa unyang’anyi na uovu. Enyi wapumbavu; aliyevifanya vya nje, siye yeye aliyevifanya vya ndania pia? Lakini, toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vyote huwa safi kwenu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


Copyright © 2024, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment