Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, OKTOBA 14, 2024




MASOMO YA MISA, OKTOBA 14, 2024
JUMATATU, JUMA LA 28 LA MWAKA


SOMO 1
Gal 4:22-24, 26-27, 31:5:1

Imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili.Mmoja alikuwa mjakazi na mwingine alikuwa muungwana. Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa muungwana kwa ahadi. Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, mmoja kutoka Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni hajiri. Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana naye ndiye mama yetu sisi. Kwa maana imeandikwa, furahi wewe uliye tasa, usiye zaa; paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu:maana watoto wakealiyeachwa pekee ni wengi kuliko huyo aliye na mume. Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazibali tu watoto wa huyo aliye mwungwana.
     
Katika ungwana huo Kristo alituandikia huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.

Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu


WIMBO WA KATIKATI
Zab 113:1-7 (K) 2

(K) Jina la bwana lihimidiwe milele

Aleluya 
Enyi watumishi wa Bwana sifuni
Lisifuni jina la Bwana
Jina la Bwana lihimidiwe
Tangu leo na hata milele. (K)

Toka mawio ya jua hata machweo yake
 Jina la bwana husifiwa
Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote
Na utukufu wake ni juu ya mbingu (K)

Ni nani aliye mfano wa bwana
Mungu wetu aketiye juu
Anyenyekeaye kutazama
Mbinguni na duniani?
Humwinua mnyonge kutoka mavumbini
Na kumpandisha masikini toka jaani. (K)


SHANGILIO
Zab 119:34

Aleluya, aleluya 
Unifahamishe nami nitaishika sheria yako
Nitaitii kwa moyo wangu wote
Aleluya 


INJILI
Lk. 11:29-32

Makutano walipokuwa wakimkusanyikia, Yesu alianza kusema, Kizazi hiki ni kizazi kibaya; kinatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya Yona. Maana, kama vile Yona alivyokuwa ishara kwa Waninawi, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu kwa kizazi hiki. Malkia wa Kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa na hatia; kwa sababu yeye alikuja kutoka nchi za dunia aisikie hekima ya Sulemani; na hapa pana mkubwa kuliko Sulemani. Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao watakihukumu kuwa na hatia; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na hapa pana mkubwa kuliko Yona.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


Copyright © 2024, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment