“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa, Novemba 1, 2024,
Juma la 30 la Mwaka wa Kanisa
Sherehe ya Watakatifu Wote
Uf 7:2-4, 9-14;
Zab 23:1-6;
1 Yn 3:1-3;
Mt 5:1-12
WATAKATIFU: WITO WA WATU WOTE WA KUWA
WATAKATIFU!
Watakatifu ni wale walio jitahidi kuishi hapa
duniani kadiri ya thamani ya Injili. Hata baada ya kifo chao wanaendelea kuwa
mfano na mashuhuda wa Injili kwa wale waliobaki dunaini. Wakiwa wameumbwa
wakiwa na mwili na damu kama sisi walitamani kupata utakatifu. Hawa ni wale
waliopata moyo kutoka kwa watakatifu wengine wakisema “kama yeye amekuwa
mtakatifu kwanini mimi nisiwe?” Watakatifu mbinguni wana bahati ya kuwa mbele
za Mungu daima. Walio wengi wakiwa bado hapa duniani walifurahia kuwa ndani ya
Mungu daima wakiwa hapa duaniani. Mginguni ni pale alipo Mungu, na Mungu yupo
ndani ya mioyo yetu, kwahiyo walikuwa na Mungu daima mbinguni. Watakatifu
waliishi wakilijua hili na wakajikuta wakiwa katika furaha ya Mungu daima.
Injili ya Leo inatualika kufuata zile heri kama
njia ya kuelekea kupata Utakatifu. Sisi ni nani tuishi maisha ya utakatifu? Mt.
Augustino alijikuta akipata ugumu wakuishi heri hizi, lakini alisoma maisha ya
watakatifu na akasema, “ Kama hawa watu wakawaida waume kwa wake waliweza,
kwanini mimi nisiweze?”
Sala: Bwana, umetuita kuwa wakamilifu kama Baba
yetu wa Mbinguni. Tuwekee ndani yetu hamu ya kukufurahisha wewe kwa kila kitu
na utufundishe njia ya ukamilifu. Amina
Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya
Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment