Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

WAPENDE MAADUI



“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Alhamisi, Septemba 12,  2024, 
Juma la 23 la Mwaka

1Kor 8: 1-7, 11-13; 
Zab 139: 1-3, 13-14, 23-24; 
Lk 6: 27-38


WAPENDE MAADUI 

Yesu aliwaambia wafuasi wake: “kwenu sikieni wapendeni maadui zenu, watendeeni mema wanao wachukia, wabarikini wanao walaani, waombeeni wanao watenda vibaya.” - Luka 6:27-28

Maneno haya ni marahisi sana kuyasema kuliko kuyatenda. Wakati watu wamekutendea vibaya kwa kukutenda vibaya unachopaswa kufanya ni kuwapenda na kuwaombea. Na Yesu anasema kwa uhakika kwamba hichi ndicho tulichoitwa kufanya. 

Katikati ya mateso na vita inayofanywa juu yetu ni rahisi kuumia. Na huku kuumia kunaweza kutufanya tupatwe na hasira na kutaka kurudisha kisasi na hata chuki. Kama tutakubali kuingia katika kishawishi hichi tutakuwa sisi wenyewe tumeamua kujiumiza. Ukweli ni kwamba kuwachukia wale waliotuumiza hufanya mambo yawe mbaya zaidi. 

Lakini tutakuwa waongo kusema ukweli kuhusu nguvu inayotusukuma kutoka ndani mwetu hasa pale tunapokosewa na inavyokuwa vigumu kutimiza maneno ya Yesu ya kurudisha kwa upendo. Ili kuwa waaminifu ni vizuri tukubali ukweli huu kwanza. Nguvu hii huondoka ndani pale tunapojaribu kushika upendo licha ya hasira na hisia tulizo nazo. 

Hisia hizi zinatujulisha kwamba Mungu anahitaji mengi zaidi kutoka kwetu na sio kuongozwa na hisia hizi. Kuwa na hasira au chuki sio kitu cha kufurahisha. Ukweli ni kwamba kinaweza kuwa ni kitendo cha mateso makubwa, lakini haipaswi kuwa hivyo. Kama tumeeelewa ujumbe huu wa Yesu njia yake ni njia nzuri ya kukwepa mateso haya. Tutatambua kwamba kulipiza kisasa hufanya kidonda kiwe kikubwa zaidi na zaidi. Tukijifunza kupenda pale mahali ambapo tumetendewa vibaya tunatambua kwamba upendo katika hali hii huwa na nguvu sana. Ni upendo ndio unaoenda zaidi ya hisia. Upendo huu tumepewa kama zawadi kutoka kwa Mungu. Ni upendo na ukarimu ndio unatufanya tuwe na furaha ya kweli..

Tafakari leo juu ya kidonda chochote kile unachokibeba ndani mwako. Tambua kwamba vidonda hivi vinaweza kuwa sababu ya utakatifu wako na furaha yako kama utamruhusu Mungu akubadilishe na kuanza kuwatendea kwa upendo wale waliokutenda mabaya. 

Sala: Bwana, ninatambua kwamba nimeitwa niwapende maadui wangu. Ninatambua kwamba nimeitwa niwapende wale wote walionitenda mabaya. Nisaidie niweze kukabidhi kwako hisia zote za chuki au hasira naomba uvibadilishe kwa upendo wa kweli. Yesu nakuamini wewe. Amina


.Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment