“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Alhamisi, Julai 11, 2024,
Tafakari ya kila siku
Juma la 14 la Mwaka wa Kanisa
Hos 11:1-4, 8-9;
Zab 79:2-3, 15-16;
Mt 10:7-15
UWEZO KATIKA UTUME!
Yesu mwana wa Mungu, alitumwa Ulimwenguni kwa Upendo wa Baba, alitangaza Ufalme wa Mungu ndani ya ufalme wa mwanadamu, ili watoke kutoka katika utawala wa yule mwovu. Akitutaka wadhambi kama mimi na wewe, tuache dhambi tushirikiane naye katika kuokoa ulimwengu kutoka katika giza la kifo na mauti, aliwachagua wafuasi kumi na wawili akawaita mitume mwazoni kabisa mwa utume wake. Kwa hawa aliwapa mafundisho maalumu kwaajili ya utume wao, akawapa uwezo wakutoa pepo, kufufua wafu na kuponya magonjwa mbali mbali.
Injili inomuonesha Yesu kama daktari mkuu, akiwaponya wenye ukoma, waliopooza, vipofu na viziwi, na hata kuwafufua wafu. Yesu, sasa anawashirikisha mitume wake nguvu hizi, ambao watakuwa mawakili wa kutangaza ufalme wa Mungu. Kama ilivyo katika elimu, mafunzo ya kijeshi, au mafunzo yeyote., inawapa watu ujuzi wa maisha, pia mitume wa Yesu walihiitaji mafundisho ili waweze kuwa na kiwango cha kutangaza Ufalme wa Mungu. Ufukara ulipaswa kuwa silaha yao dhidi ya hekima ya ulimwengu, na Amani ilipaswa kuwa matunda ya hekima yao. Walipaswa wamtegemee Mungu na pia kwa msaada wa waliowapa watu. Hii ni jinsi ghani Yesu alivyojua vizuri pesa ni chanzo cha maovu mengi.
Ni kwa jinsi ghani wakati mwingine Kanisa limedhoofishwa katika utume wake kwasababu ya kuwa dhaifu katika pesa, pengine utajiri na tamaa. Uwezo wa Kanisa unakuja kwa ufukara wake na misaada ambapo unyenyekevu wa kweli ndio msingi wake. Chanzo kingine cha uwezo wa utume ni Amani ya ndani na utulivu unaotoka katika dhamira iliyo safi na yenye unyenyekevu wa kweli. Mtume wa kweli anabaki mtulivu pale anapo kubaliwa au kukataliwa.
Sala: Roho Mtakatifu, tunaomba utufanye Wakristo wapya, na zaidi sana watumishi wako makleri waweze kuwa mitume wa kweli siku zote. Amina.
Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment