JUMAMOSI
YA 15 YA MWAKA
SOMO
YA 1
Mik.
2:1 – 5
Ole
wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao! Kunapopambazuka
asubuhi huyafanya, kwa sababu ya katika uwezo wa mikono yao. Nao hutamani
mashamba, na kuyashika; na nyumba pia, nao huzichukua; nao humwonea mtu na
nyumba yake, naam, mtu na urithi wake. Basi Bwana asema hivi, Angalia,
nakusudia jambo baya juu ya jamaa hii, ambalo hamtazitoa shingo zenu, wala
hamtakwenda kwa kiburi; kwa maana ni wakati mbaya. Siku hiyo watatunga mithali
juu yenu, na kuomboleza kwa maombolezo ya huzuni nyingi, na kusema, Sisi
tumenyang’anyiwa kabisa; Yeye analibadili fungu la watu wangu; Jinsi
anavyoniondolea hilo!
Awagawia
waasi mashamba yetu. Kwa hiyo hutakuwa na mtu atakayeitupa Kamba kwa kura
katika mkutano wa Bwana.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
10:1 – 4, 7 – 8, 14 (K) 12
(K)
Usiwasahau wanyonge, Ee Bwana.
Ee
Bwana, kwa nini wasimama mbali?
Kwa
nini kujificha nyakati za shida?
Kwa
kiburi chake asiye haki
Mnyonge
anafuatiwa kwa ukali;
Na
wanaswe kwa hila zizo hizo walizoziwaza. (K)
Maana
mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake,
Na
mwenye choyo humkana Bwana na kumdharau.
Mdhalimu
kwa kiburi cha uso wake
Asema,
Hatapatiliza.
Jumla
ya mawazo yake ni, Hakuna Mungu. (K)
Kinywa
chake kimejaa laana,
Na
hila na dhuluma.
Chini
ya ulimi wake kuna madhara na uovu,
Hukaa
katika maoteo ya vijivi.
Mahali
pa siri humwua asiye na hatia,
Macho
yake humvizia mtu duni. (K)
Umeona,
maana unaangalia madhara na jeuri,
Uyatwae
mkononi mwako.
Mtu
duni hukuachia nafsi yake,
Maana
umekuwa msaidizi wa yatima. (K)
SHANGILIO
Yn.
14:23
Aleluya,
aleluya,
Mtu
akinipenda, atalishika neno langu, na Baba yangu atampenda, na sisi tutakuja
kwake.
Aleluya.
INJILI
Mt.
12:14 – 21
Mafarisayo
walitoka wakafanya shauri juu ya Yesu jinsi ya kumwangamiza. Naye Yesu hali
akiyafahamu hayo akaondoka huko; na watu wengi wakamfuata; akawaponya wote,
akawakataza wasimdhihirishe; ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya,
akisema,
Tazama,
mtumishi wangu niliyemteua; mpendwa wangu, moyo wangu uliyependezwa naye;
nitatia roho yangu juu yake, naye atawatangazia Mataifa hukumu. Hatateta wala
hatapaza sauti yake; wala mtu hatasikia sauti yake njiani. Mwanzi uliopondeka
hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima, hata ailetapo hukumu ikashinda.
Na jina lake Mataifa watalitumainia.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2024, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment