MASOMO
YA MISA, JULAI 19, 2024
IJUMAA
YA 15 YA MWAKA
SOMO
1
Isa.
38:1 – 6, 21 – 22, 7 – 8
Siku
hizo Hezekia aliugua, akawa katika hatari ya kufa; na Isaya nabii, mwana wa
Amozi, akaenda kwa mfalme, akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeneza mambo ya
nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona. Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza
uso wake ukutani, akamwomba Bwana, akasema, Ee Bwana, kumbuka haya, nakusihi
kwamba nimekwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda
yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.
Kisha
neno la Bwana likamjia Isaya, kusema, Enenda ukamwambie Hezekia, Bwana, Mungu
wa Daudi, baba yako, asema hivi, Mimi nimeyasikia maombi yako, nimeyaona
machozi yako; tazama nitaziongeza siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano.
Nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, name nitaulinda
mji huu.
Basi
Isaya akasema, Na watwae mkate wa tini, wakauweke juu ya jipu, naye atapona.
Tena Hezekia alikuwa amesema, Iko ishara gani ya kunionyesha ya kuwa nitapanda
niingie nyumbani mwa Bwana? Jambo hili liwe ishara kwako itokayo kwa Bwana, ya
kuwa Bwana atalitimiza jambo hili alilolisema; Tazama, nitakirudisha nyuma
kivuli madaraja kumi, ambayo kilishuka juu ya duara ya Ahazi kwa sababu ya jua.
Basi jua likarudi madaraja kumi katika hiyo duara, ambayo limekwisha kushuka.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Isa.
38:10 – 12, 16 (K) 17
(K)
Umeniokoa na shimo la uharibifu, Ee Bwana.
Nalisema,
katika usitawi wa siku zangu
Nitakwenda
kuingia malango ya kuzimu;
Nimenyimwa
mabaki ya miaka yangu. (K)
Nalisema,
Sitamwona Bwana, yeye Bwana,
Katika
nchi ya walio hai;
Sitamwona
mwanadamu tena pamoja na hao
Wakaao
duniani. (K)
Kao
langu limeondolewa kabisa,
Limechukuliwa
kama hema ya mchungaji;
Nimekunja
maisha yangu kama mfumaji;
Atanikatilia
mbali na kitanda cha mfumi;
Tangu
mchana hata usiku wanimaliza. (K)
Ee
Bwana, kwa mambo hayo watu huishi;
Na
uhai war oho yangu u katika hayo yote;
Kwa
hiyo uniponye na kunihuisha. (K)
SHANGILIO
Yn.
10:27
Aleluya,
aleluya,
Kondoo
wangu waisikia sauti yangu, name nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
INJILI
Mt.
12:1 – 8
Wakati
ule Yesu alipita katika mashamba siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa,
wakaanza kuvunja masuke, wakala. Na Mafarisayo walipoona, walimwambia, Tazama!
Wanafunzi wako wanafanya neno ambalo si halali kulifanya siku ya sabato.
Akawaambia,
Hamkusoma alivyotenda Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wenziwe? Jinsi
alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si
halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao? Wala
hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi
sabato wasipate hatia? Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko
hekalu. Lakini kama mngalijua maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si
sadaka, msingaliwalaumu wasio na hatia. Kwa maana Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa
sabato.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2024, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
Tumsifu Yesu Kristo.....
ReplyDeleteNaomba unisaidie jina sahihi la kiume kwa mtoto aliyezaliwa siku hii ya Julai 19
Tumsifu Yesu Kristo.....