MASOMO
YA MISA, JULAI 18, 2024
ALHAMISI
YA 15 YA MWAKA
SOMO
1
Isa.
26:7 – 9, 12, 16 – 19
Njia
yake mwenye haki ni unyofu; wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki.
Naam, katika njia ya hukumu zako sisi tumekungoja, Ee Bwana; shauku ya nafsi
zetu inaelekea Jina lako na ukumbusho wako.
Kwa
nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; naam, kwa nafsi yangu ndani yangu
nitakutafuta mapema; maana hukumu zako zikiwapo duniani, watu wakaao duniani
hujifunza haki.
Bwana,
utatuamuria Amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote. Bwana,
katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu ayko
ilipokuwa juu yao.
Kama
vile mwanamke mwenye mimba anayekaribia wakati wake wa kuzaa, alivyo na utungu
na kulia kwa sababu ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa sisi mbele zako, Ee
Bwana. Tumekuwa na mimba, tumekuwa na utungu, tumekuwa kana kwamba tumeza
upepo; hakutkufanya wokovu wowote duniani, wala hawakuanguka wakaao duniani.
Wafu
wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa
mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa
waliokufa.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
102:12 – 20 (K) 19
(K)
Toka mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Wewe,
Bwana, utaketi ukimiliki milele,
Na
kumbukumbu lako kizazi hata kizazi.
Wewe
mwenyewe utasimama,
Na
kuirehemu Sayuni,
Kwa
maana ndio wakati wa kuihurumia,
Naam,
majira yaliyoamriwa yamewadia.
Maana
watumishi wake wameyaridhia mawe yake;
Na
kuyaonea huruma mavumbi yake. (K)
Kisha
mataifa wataliogopa jina la Bwana,
Na
wafalme wote wa dunia utukufu wake.
Bwana
atakapokuwa ameijenga Sayuni,
Atakapoonekana
katika utukufu wake.
Atakapoyaelekea
maombi yake aliye mkiwa,
Asiyadharau
maombi yao. (K)
Kizazi
kitakachokuja kitaandikia hayo,
Na
watu watakaoumbwa watamsifu Bwana.
Maana
ametazama toka patakatifu pake pa juu,
Toka
mbinguni Bwana ameangalia nchi.
Ili
akusikie kuugua kwake aliyefungwa,
Na
kuwafungua walioandikiwa kufa. (K)
SHANGILIO
Zab.
111:7, 8
Aleluya,
aleluya,
Maagizo
yako yote, ee Bwana, ni amini, yamethibitika milele na milele.
Aleluya.
INJILI
Mt.
11:28 – 30
Yesu
aliwaambia makutano: Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na
mizigo, name nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi
ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; kwa maana
nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2024, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment