MASOMO YA MISA - TAREHE, JUNI 2, 2024 (MWAKA B)
SHEREHE YA MWILI NA DAMU TAKATIFU YA BWANA WETU YESU KRISTO
SOMO 1
Kut. 24 : 3-8
Musa alienda akawaambia watu maneno vote ya Bwana, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena Bwana tutayatenda. Basi Musa akayaandika maneno yote ya Bwana, akaondoka asubuhi na mapema; akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya kabila kumi na mbili za Israeli, akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia Bwana sadaka za amani za ng’ombe. Musa akatwaa nusu ya ile damu, akatia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainvunyiza juu ya madhabahu. Kisha akakitwaa kitabu cha agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena Bwana tutayatenda, nasi tutatii. Musa akakitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maneno haya yote.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 116:12-13, 15-18 (K) 13
(K) Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza jina la Bwana.
Nimrudishie Bwana nini
Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
Nitakipokca kikombe cha wokovu;
Na kulitangaza jina la Bwana. (K)
Ina thamani machoni pa Bwana
Mauti ya wacha Mungu wake.
Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako,
Umevifungua vifungo vyangu. (K)
Nitakutolea dhabihu ya kushukuru;
Na kulitangaza jina la Bwana;
Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana,
Naam mhplf va watu wake wote. (K)
SOMO 2
Ebr. 9:11-15
Kristo aliisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Kwa maana ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng’ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hai?
Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
SEKWENSIA - EE SAYUNI UMTUKUZE
Ee Sayuni umtukuze,
Uwezavyo umwimbie,
Mukombozi na Mwalimu
Apitaye kila sifa,
Kwa nyimbo na shangwe kuu,
Itokayo kwa watu.
Nia yetu ya kusifu,
Lisho hili walipewa
Hasa mkate mtakatifu,
Wale kumi na wawili,
Uletao uzima,
Karamuni mwa mwisho.
Shangilio la rohoni,
Lipendeze liwe zuri,
Sifa tele livume.
Ipo leo siku kubwa,
Kwa kumbusho la kuwekwa,
Kwanza ile karamu.
Muda ule umekwisha,
Ipo meza ya Mufalme,
Na sheria mpya.
Tumepata mapya yote,
Nuru, siyo nusu giza
Mwanga siyo usiku.
Tendo lake karamuni,
Kristu ametuamuru
Tutende tumkumbuke.
Twafuata amri yake,
Tukitoa hii sadaka,
Kwa mkate na divai.
Mkate wageuka Mwili,
Na divai ikawa Damu,
Kanuni kwa wakristu.
Huelewi huioni,
Kweli hiyo; ukubali
Maana ni mwujiza mkuu.
Unaona tu maumbo;
Ni alama zifumbazo,
Utukufu wenyewe.
Ule Mwili, unywe Damu
Kila umbo linamfumba,
Yesu mzima halisi.
Ukipewa tu kimego,
Umempata Yesu mzima,
Si sehemu yake tu.
Mmoja hula, elfu hula,
Wote hupokea sawa,
Na mpokewa hakomi.
Hula wema na wabaya,
Kwa bahati mbalimbali,
Kifo au uzima.
Basi, mkate mtakatifu
Huwa sumu kwa wabaya,
Dawa bora kwa wema.
Ikimegwa sakramenti,
Usisite, uamini:
Huwa ndani ya kipande
Mwili wote wa Yesu
Mwili wake haumegwi,
Ni alama ivunjwayo,
Hali yake pia kimo cha
Mwenyewe ni sawa.
Kumbe mkate wa Malaika,
Huwalisha wasafiri,
Kweli mkate wa wana
usitupwe kwa mbwa.
Hii mifano ya zamani,
Kutolewa mwana Isak,
Na kondoo kuchinjwa Paska,
pia mana ya jangwani.
Ee Mchungaji wetu mwema,
Yesu utuhurumie,
Utuchunge, utulinde.
Ee Mchungaji wetu mwema,
Tuonyeshe mema yako,
Huko kwenye wazima.
Ee Mchungaji wetu mwema,
Ee Mwenyezi na Mjuaji,
Mwenye kutuchunga hapa:
Tujalie pia huko,
Kushiriki meza moja,
Na raia wa mbinguni. Amina.
SHANGILIO
Yn. 6 :51
Aleluya, Aleluya,
Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; asema Bwana;
mtu akila chakula hiki, ataishi milele.
Aleluya.
INJILI
Mk. 14 :12-16, 22-26
Siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Ni wapi utakapo tuende tukuandalie uile pasaka? Akatuma wawili katika wanafunzi wake, akawaambia, Nendeni zenu mjini; atakutana nanyi mwanamume amechukua mtungi wa maji; mfuateni; na po pote atakapoingia, mwambieni mwenye nyumba, Mwalimu asema, Ki wapi chumba changu cha wageni, niile pasaka humo, pamoja na wanafunzi wangu? naye mwenyewe atawaonyesha orofa kubwa, imeandikwa tayari; humo tuandalieni. Wanafunzi wakatoka, wakaenda mjini, wakaona kama alivyowambia. wakaiandaa pasaka.
Nao walipokuwa wakila, alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa akisema, Twaeni; huu ndio mwili wangu. Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote. Akawaambia, Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. Amin, nawaambia ninyi, Sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu. Nao walipokwisha kuimba walitoka kwenda mlima wa Mizeituni.
Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2024, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment