MASOMO YA MISA, JUNI 17, 2026
JUMATANO, JUMA LA 11 LA MWAKA
SOMO 1
1 Fal. 2:1, 6-14
Bwana lipopenda kumpandisha
Eliya mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya alitoka Gilgali pamoja na Elisha.
Eliya akamwambia, Tafadhali kaa hapa; maana bwana amenituma niende mpaka
Yordani. Akasema, kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Wakaendelea
mbele wote wawili.
Basi watu hamsini wa wale wana
wa manabii wakaenda wakasimama, kuwakabili kwa mbali; na hao wawili wakasimama
karibu na Yordani. Eliya akalitwaa vazi lake la juu, akalikunja, akayapiga
maji, yakagawanyika huku na huku, na hao wawili wakavuka pakavu. Hata ikawa,
walipokwisha kuvuka, Eliya akamwambia Elisha, Omba kwangu lolote utakalo
nikutendee, kabla sijaondolewa kwako. Elisha akasema, Nakuomba, sehemu maradufu
ya roho yako na iwe juu yangu. Akasema, Umeomba neno guvu; lakini, ukiniona
nitakapoondolewa kwako, utalipata; la, hukuniona, hulipati. Ikawa walipokuwa
wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kutatokea gari la moto, na farasi wa
moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa
kisulisuli. Naye Elisha akaona, akalia, Baba yangu, baba yangu, gari la
Israeli na wapanda farasi wake! Asimwone tena kabisa; akashika mavazi yake
mwenyewe, akayararua vipande viwili. Kisha akaliokota lile vazi la Eliya
lililomwangukia, akarudi, akasimama katika ukingo wa Yordani.
Akalitwaa lile vazi la Eliya
lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko wapi Bwana, Mungu wa Eliya? Naye
laipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka.
Akalitwaa lile vazi la Eliya
lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko wapi Bwana, Mungu wa Eliya? Naye
laipoyapiga maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha akavuka.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 31:19, 20, 23 (K) 24
(K) Iweni hodari, mpige moyo
konde, ninyi nyote mnaomngoja Bwana.
Jinsi zilivyo nyingi fadhili
zako
Ulizowawekea wakuchao;
Uulizowatendea wakukimbiliao
Mbele ya wanadamu! (K)
Utawasitiri na fitina za watu
Katika sitara ya kuwapo kwako.
(K)
Mpendeni Bwana,
Ninyi nyote mlio watauwa wake.
Bwana huwahifadhi waaminifu,
Humlipa atendaye kiburi malipo
tele. (K)
SHANGILIO
1 Pet. 1:25
Aleluya, aleluya,
Neno la Bwana hudumu hata
milele, na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.
Aleluya.
INJILI
Mt. 6:1-6, 16 – 18
Yesu aliwaambia wanafunzi wake;
Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana
mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni. Basi wewe
utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika
masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha
kupata thawabu yao. Basli wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue
ufanyalo mkono wako wa kuume; sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye
sirini atakujazi.
Tena msalipo, msiwe kama wanafiki;
kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe
za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.
Bali wewe usalipo, ingia katika chumba cha
ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye
sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Tena mfungapo, msiwe kama
wanfiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao; ili waonekane na
watu kuwa nafunga, Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe ufungapo,
jipake mafuta kichwani, unawe uso; ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na
Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2026, "MASOMO
YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:
Post a Comment