
MASOMO YA MISA, JUNI 16, 2026
JUMANNE, JUMA LA 11 LA MWAKA
SOMO 1
1 Fal. 21:17-29
Neno la Bwana likamjia Eliya
Mtishbi, kusema, Ondoka, ushuke, ukutane na Ahabu mfalme wa Israeli, akaaye
katika Samaria; yuko katika shamba la mizabibu la Nabothi, ndiko alikoshukuia
ili alitamalaki. Ukamwambie, ukisema, Bwan aasema hivi, Je! Umeua, ukatamalaki?
Nawe utamwambia, kusema, Bwana asema hivi, mahali pale mbwa walipoiramba damu
ya Nabothi, mbwa watairamba na damu yako, naam, damu yako.
Ahabu akamwambia Eliya, Je!
Umenipata, ewe adui yangu? Akamwambia, Nimekupata, kwa sababu umejiuza utende
yaliyo mabaya machoni pa Bwana. Angalia, nitaleta mabaya juu yako; nami
nitakuangamiza kabisa, nitamkatia Ahabu kila mume, aliyefungwa na aliyeachwa
katika Israeli.
Kisha nitaifanya nyumba yako
iwe kama nyumba ya Yeroboamu mwana wa Nebari, na kama nyumba ya Baasha mwana wa
Ahiya, kwa ajili ya chukizo ulilonichukiza, hata kunighadhibisha, ukawakosesha
Israeli. Tena Bwana alinena habari za Yezebeli, akisema, Mbwa watamla Yezebeli
katika kiwanja cha Yezreeli. Mtu wa nyumba ya Ahabu afanye mjini, mbwa watamla,
na yeye afaye mashamba ndege wa angani watamla.
Lakini hapakuwa na mtu kama
Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa Bwana, ambaye Yezebeli mkewe
alimchochea. Akachukiza mno, kwa kuzifuata sanamu sawasawa na yote
waliyoyafanya Waamori, Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli.
Ikawa, Ahabu alipoyasikia
maneno hayo, akayararua mavazi yake, akavaa magunia mwilini mwake, akafunga,
akajilaza juu ya magunia, akaenda kwa upole. Neno la Bwana likaja kwa Eliya
Mtishbi, kusema, Huoni jinsi Ahabu alivyojidhili mbele yangu? Basi kwa sababu
amejidhili mbele yangu, sitayaleta yale mabaya katik asiku zake; ila katika
siku za mwanawe nitayaleta mabaya hayo juu ya nyumba yake.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 51:1-4, 9, 15 (K) 1
(K) Ee Mungu uturehemu uyafute
makosa yetu.
Ee Mungu unirehemu, sawasawa na
fadhili zako.
Kiasi cha wingi wa rehema zako,
Uyafute makosa yangu.
Unioshe kabisa na uovu wangu,
Unitakase dhambi zangu. (K)
Maana nimejua mimi makosa
yangu,
Na dhambi yangu i mbele yangu
daima.
Nimekutenda dhambi Wewe peke
yako. (K)
Usitiri uso wako usitazame
dhambi zangu,
Uzifute hatia zangu zote.
Ee Bwana, uifumbue midomo
yangu,
Na kinywa hcangu kitazinena
sifa zako. (K)
SHANGILIO
Yak. 1:21
Aleluya, aleluya.
Pokeeni kwa upole neno la mungu
lililopandwa ndani, liwezalo kuiokoa roho zenu.
Aleluya.
INJILI
Mt. 5:43 – 48
Yesu aliwaambia wanafunzi wake:
Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, pendeni adui zenu, waombeeni
wanaowaudhi; ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye
huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyk, mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru;
je! Nao hawafanyi yayo hayo? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani
la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? Basi ninyi mtakuwa
wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2026, "MASOMO
YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment