Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MATUNDA YENYE KUWAVUTA WATU


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa, Juni, 2, 2023
Tafakari ya kila siku
Juma la 8 la mwaka wa Kanisa

Ybs 44:1, 9-13; 
Zab 149:1-6, 9; 
Mk 11: 11-26


MATUNDA YENYE KUWAVUTA WATU


Yesu alivyo ulaani mtini baada ya kuuona hauna matunda, kitendo hiki kinaweza kuonekana cha ajabu kidogo na cha kutisha. Yesu alijua kabisa ilikuwa sio kipindi cha matunda ya mti ule. Mt. Beda katika maelezo yake akiongelea kuhusu muujiza huu wa Yesu, anatuambia kwamba, muujiza huu wa Yesu ulikuwa na lengo maalumu. Yesu alikuja kati ya watu wake, Wayahudi, akiwa na njaa yakutaka matunda ya utakatifu, wao hawakuupokea ujumbe wake na matunda ya kazi yake. Lakini yote aliyo yakuta ni msisitizo wakushika dini, matendo ya njee yasioendani na kilicho ndani, na katika hali hii wamekuwa kama majani ya miti bila matunda. Wakati alivyo ingia Hekaluni alikuta wamepageuza kuwa pango la biashara. Kitu ambacho kilimfanya hata halitakase kwakutumia nguvu. “Kwahiyo wewe” anasema Mt. Beda kwakumalizia, “unapaswa ujilinde usiwe kama mti usio zaa matunda, jitoe kwa Yesu, aliyejifanya mwenyewe maskini, anategemea uwe tunda la utakatifu” 

Fadhila zinaongeza furaha ya maisha ya sala na sala inapaswa ionekane katika matendo ya fadhila. Sala ya kweli inapaswa utuongoze taratibu katika mabadiliko ya kweli ya maisha yetu, tukikua katika fadhila na madiliko ya ndani. Vinginevyo tutakuwa kama Wayahudi, mtini uliyo na majani pekee usio zaa matunda.

Sala: Bwana nijaliye neema, ili kwa maisha yangu niweze kutoa matunda mema. Amina.

Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment