Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA TANO: JUMANNE BAADA YA PASAKA




NOVENA YA HURUMA YA MUNGU
SIKU YA TANO: JUMANNE BAADA YA PASAKA


NAMNA YA KUFANYA NOVENA KWA HURUMA YA MUNGU

Sala ya kutubu:
Mungu wangu, ninatubu sana dhambi zangu, kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza, wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena, nitafanya kitubio, naomba neema yako nipate kurudi kwako, Amina.

Nia ya sala za leo:
SIKU YA TANO

Maneno ya Mkombozi: “Leo niletee roho za ndugu waliojitenga na Kanisa, na uwazamishe katika Bahari Kuu ya Huruma yangu. Wakati ule wa mateso yangu makali, watu hawa waliurarua mwili wangu na roho yangu, yaani Kanisa langu. Pindi warudipo tena katika Umoja wa Kanisa, majeraha yangu hupona, na kwa njia hii wanapunguza ukali wa mateso yangu”.

Tuwaombee wale waliopotoka katika Imani Katoliki na kujitenga na Kanisa.

W. Ee Yesu Mpole na mwenye Huruma, Wewe u Huruma na Wema wenyewe, hukatai kuwapa mwanga wale wote wanaoutafuta. Uzipokee ndani ya Moyo wako wenye Huruma, roho za ndugu zetu waliojitenga. Uwavute kwa mwanga wako, ili warudi tena katika Umoja wa Kanisa lako Takatifu, na uwadumishe humo, wasiweze kutoroka tena Moyo wako wenye Huruma sana, bali uwawezeshe wao pia pamoja nasi, kuusifu na kuutukuza ukarimu wa Huruma Yako Kuu, kwa milele na milele. Amina.

Baba yetu ……. Salamu Maria …….. Atukuzwe …………..

W. Baba wa Milele, uzielekee kwa macho ya huruma, roho za ndugu zetu waliojitenga na Kanisa lako Takatifu, hasa wale waliozitapanya Baraka zako na kuzitumia vibaya neema zako, kwa kuendelea kishupavu katika mafundisho yao ya upotofu. Usiyaangalie hayo makosa yao, bali uutazame upendo wa Mwanao Mpenzi, pamoja na mateso yake makali aliyovumilia kwa ajili yao. Watu hawa pia, wameingizwa ndani ya Moyo wa Yesu Mwanao, wenye Huruma Kuu. Uwawezeshe vile kwamba, wao pamoja na sisi sote, tuisifu na kuitukuza Huruma Yako Kuu, kwa milele na milele. Amina.

Rozari  ya Huruma ya Mungu
(Tumia chembe za rozari ya kawaida)
Baba yetu …       Salamu Maria …. x3            Nasadiki kwa Mungu Baba Mwenyezi …….

Kwenye chembe kubwa
Baba wa Milele, ninakutolea Mwili na Damu, Roho na Umungu, wa Mwanao Mpenzi sana, Bwana wetu Yesu Kristu, kwa ajili ya malipizi ya dhambi zetu, na dhambi za dunia nzima.

kwenye chembe ndogo
Mwanzishaji: Kwa ajili ya mateso makali ya Bwana wetu Yesu Kristo,
Wote huitika: Utuhurumie sisi na dunia nzima.

Mwisho wa Rozari sali mara tatu sala ifuatayo:
Mungu Mtakatifu, Mtakatifu mwenye Enzi, Mtakatifu unayeishi milele, Utuhurumie sisi na dunia nzima.


Litania ya Huruma ya Mungu

No comments:

Post a Comment