“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya Pasaka
Jumamosi, Aprili 27, 2024.
Juma la 4 la Pasaka
Mdo 13:44-52;
Zab 98:1-4 (R. 3);
Yn 14:7-14.
MUNGU KUDHIHIRIKA NDANI YA MAISHA YETU!
Mara nyingi, hatujui ni kwa jinsi ghani Mungu anajifunua mwenyewe katika maisha yetu kama Filipo, anayetaka kumuona Baba. Alikuwa mbele ya Yesu, na bado anamtafuta Mungu. Sisi pia katika maisha yetu. Mungu yupo nasi daima lakini kwasababu ya mawazo yetu na mitizamo yetu tunamtafuta. Sisi nasi tunamtafuta Mungu na baadae tuna mtambua Yesu mbele yetu.
Paulo na Baranabas walitambua utambulisho wa kweli wa Yesu na wanamhubiri kwa ujasiri mkubwa, kwa mataifa licha ya mateso na vipingamizi. Kama sisi tunajiita wakristo, Kristo anapaswa kudhihirika katika maisha yetu. Kama kumuona Yesu ni kumuona Mungu Baba ni wazi kwa matumaini na katika sala, kutuona sisi ni kumuona Yesu pia.
Injili ya Yohane inatumia lugha hii mara nyingi kuonesha umoja mkamilifu wa Yesu na Baba yake. Ni jambo zuri namna ghani sisi nasi kusema sisi hatuseme wenyewe bali ni Kristo anasema ndani yetu? Hili ndilo linalopaswa kuwa lengo letu la kila mara. Kama tutaongea maneno kwa wengine, tukiwa tumejikita katika hekima yetu wenyewe na uelewa wetu wenyewe, ni lazima tuji nyenyekeshe na kutambua kwamba maneno yetu hayawezi kuwa na nguvu. Lakini kwa upande mwingine, lakini kama tunaweza kusema maneno yaliyo jaa Kristo, maneno ambayo yanasemwa kutoka ndani ya moyo wake, tutaanza kuona maneno hayo yanakuwa na manufaa katika maisha ya watu. Maneno yana maana sana, na tunapaswa kuwa makini katika kuongea na kuwa na ujasiri na kile tunachosema, jinsi ya kusema na tunasemaje. Kumruhusu Baba aongee ndani mwetu na kupitia sisi maneno yetu yanakuwa na ujasiri na nguvu. Yanakuwa maneno ambayo Mungu alitaka kuongea kwa wengine ambayo yanamfanya Mungu afanye mabadiliko katika maisha yao.
Sala: Bwana, nipe maneno yako ya kuongea. Nisaidie mimi nikurudie wewe ndani ya moyo wangu kwa ujasiri ili uweze kuwa chanzo cha ukweli na uzuri. Ninaomba ukweli huo utoke ndani mwangu kila siku. Ninaomba wote wakuone wewe kwa njia ya maisha yangu. Yesu nakuamini wewe. Amina.
Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment