Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

WAKATI MUNGU AKIWA KIMYA


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Januari 12 2024 
------------------------------------------------

IJUMAA, JUMA LA 1 LA MWAKA

Somo la 1: 1 Sam 8:4-7,10-22 Israeli wanataka Mfalme wao, wanakataa utawala wa Mungu.

Wimbo wa katikati: Zab 88: 16-19 Wanafuraha wanao kukiri wewe Ee Bwana kuwa Mfalme, wanaotembea katika mwanga wa uso wako.

Injili : Mk 2:1-12 Yesu anamponja mtu aliyepooza waliye mpitisha juu ya dari.

------------------------------------------------

WAKATI MUNGU AKIWA KIMYA


Leo tunasikia mapinduzi katika historia ya wana Waisraeli. Watu wanataka Mfalme. Samueli anakataza kuhusu hili, kwani anatambua kwamba kumtaka Mfalme ni sababu ya ukosefu wa Imani kwa Bwana (Yahweh). Wanataka kuwa kama mataifa mengine, na anawapa kadiri ya ombi lao, bila ya kuwaambia matokeo na gharama watakayo kutana nayo kwasababu ya uchaguzi wao. Uhuru ndio Mungu anaopenda kumpa mwanadamu daima, kwani anajua kama hatupo huru kuchagua hatutakuwa huru kupenda. Na hivyo kwa uhuru alihitaji upendo wao kwake kuliko kitu kingine.

Yesu anawavuta watu kwake. Kuna watu wengi wanakuja kwa Yesu kiasi kwamba hakukuwa na nafasi kwa kila mmoja, hata katika mlango wakuingia ndani alikokuwa. Tunaweza kuwa na hakika kwamba wote waliokuja kumsikiliza hata kama hawakuweza kuingia ndani, walipata baraka kwa Imani yao. Inafunua hamu ya kiroho ya kuwa karibu na Yesu, na kuwa naye, huleta mabadiliko. Inawezekana anatokea kwetu katika ukimya au tunaweza tusifahamu tunamtafuta wapi. Lakini usikate tamaa kama hali hii imekuwa katika maisha. Ukweli ni kwamba hamu yako ya kuwa na Mungu yenyewe ni zawadi kubwa, na ina mengi ya kubadili maisha yako. 

Kuna nyakati katika maisha unahisi Mungu kuwa mbali, na mkimya na hujui pa kumpata. Wakati hili linatokea, tutambue kuwa huu ndio muda wa kuja karibu zaidi na Mungu kuliko siku nyingine zozote. Ni wakati ambao Mungu anataka kutunongoneza ili tuweze kuwa na umakini wetu tena. Muda huo weka umakini wako kwa Bwana zaidi na weka nia yako zaidi ya kutaka kuwa naye na kukuwa. Ni hamu hii ya kuwa karibu zaidi na Yesu inaweza kuleta matunda mema zaidi katika maisha yako hata zaidi kuliko ungemsikia kwa sauti kubwa zaidi.

Katika Injili tunaona uponyaji wa yule mwenye kupooza unamfanya Yesu apate upinzani. Yesu ambaye ni mwenye nguvu katika maneno na matendo, uwezo wake wa kusamehe dhambi unathibitishwa na uwezo wake wa kuponya mtu aliyepooza. Yesu ambaye ni Masihi, mtawala wa kweli na Mfalme wa Israeli, Mwana wa Mungu amekataliwa.

Katika maisha yetu pia, sisi tunafurahi tukiwa katika utumwa wa dhambi, nguvu, milki na anasa, badala ya kuwa katika uhuru wa kuachana na mambo hayo. Tuko tayari kukataa furaha ya milele kwa ajili ya kitu cha muda mfupi na cha haraka. Leo, Yesu anatuhimiza tumchague yeye kuliko yote tunayoyapenda. Je! Tunayo Imani ya kukataa yote yanayotutenga na Mungu kwaajili ya Yesu?

Sala: Bwana, naomba unifanya mimi niwe na uwezo wa kukuchagua wewe kuliko yote yanayopita ya Ulimwengu huu. Ongeza hamu yangu ya kutaka kuwa karibu nawe zaidi. Nisaidie nikutamani wewe zaidi ya yote. Nisaidie niache yote ambayo yananiweka mbali nawe na naomba nikupe umakini wangu wote. Yesu nakuamini wewe. Amina


Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment