Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MAMA MARIA, MZIMAMIZI WETU NA KIONGOZI WETU!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Januari 1, 2024
------------------------------------------------
JUMATATU, OKTAVA YA NOELI

Sherehe ya Bikira Maria Mama wa Mungu

Somo la 1: Hes 6: 22-27 Bwana anamwambia Musa na Aroni ni jinsi gani anataka watu wake wabarikiwe. 

Wimbo wa Katikati Zab 66:2-3.5-6,8 Bwana atupe Baraka zake, mpaka hapo miisho yote ya dunia watakapo mwabudu. 

Somo la 2: Gal 4:4-7 Mt. Paulo anatukumbusha juu ya utu wetu ulivyo mkubwa kwa kuwa wamoja ndani ya Kristo: sisi ni watoto wa Mungu, sio watumwa.

Injili: Lk 2: 16-21 Wachungaji wanamtembelea mtoto Yesu akiwa katika hori. Wachungaji baada ya kumuona Yesu, wanarudi kwa furaha wakimtukuza Mungu. Na Maria aliyaweka haya moyoni mwake. 

------------------------------------------------

MAMA MARIA, MZIMAMIZI WETU NA KIONGOZI WETU! 

Kila sherehe ya Maria ni ya Yesu, kwasababu Maria aliishi kwa ajili yake na kuchukuwa maana yake halisi kutoka kwa Yesu. Katika hali ya mshangao, Maria ni sababu ya Yesu kupata mwili na Yesu ni sababu ya Maria kupata hali ya Utakatifu wa mama wa Mungu. Oktava ya Noeli isingekuwa na maana kama tusingechukua siku moja kwa ajili ya Mama Maria. Hivyo tunasheherekea Maria kuwa Mama wa Yesu na hali yake ya utakatifu ya kuwa Mama wa Kanisa na hivyo katika uhalisia kuitwa “Mama wa Mungu”, na hivyo tunakiri uhalisia wa maisha ya kibinadamu. Mama sio tu sababu ya mtoto kupata mwili na wala sio Mama wa mwili wa watoto wake, ni Mama wa huyo mtu pia. Kuwa Mama sio kitu tu cha kibayogia, ni kitu Kitakatifu na cha pekee na ni sehemu ya Mungu kwa uumbaji wake. Yesu ni Mwana wake na Yesu ni Mungu. Hivyo ni mantiki kabisa kumuita Maria ni “Mama wa Mungu”. 

Mungu ana Mama! Ana mtu maaliumu aliyembeba tumboni mwake, aliyemlisha, kumtunza na kumkuza, na alikuwa pale kwa nyakati zote na kutafakari moyoni mwake ya kuwa yeye ni nani. Injili inasema kwamba “Maria aliyaweka haya yote moyoni mwake”.  Mapendo yake kwa Yesu yalikuwa ya pekee kama yalivyo mapendo ya Mama yeyote, kwa yeye ambaye hakuwa Mwana wake tu bali alikuwa Mungu katika ukamilifu wote. Yeye ni mfano kwa kila Mama na mfano kwa mapendo kwa wengine kwa ukamilifu wa moyo. 

Katika somo la kwanza, Baraka kwa watu wa Mungu ilimaanisha tumaini kwa watu. Leo pia tunaitwa tumtegemee Mungu na Baraka zake hasa tunapo anza mwaka mpya. Katika somo la pili Paulo anatupa tumaini kwa kuanza mwaka mpya: Yesu Kristo Mwana wa Mungu yeye ambaye amekuwa sawa na sisi, amekuwa ndugu kwetu kwa kila kitu isipokuwa kuwa na dhambi. Mungu ametupokea sisi kama watoto wake. Sisi wakristo tunapaswa kushuhudia upendo wa Mungu ulio oneshwa kwetu kwa njia ya Kristo. Mama kanisa daima anatukumbusha hili, kwamba tunahitaji mfano wetu wa kufuaat kwa kipindi chote cha Mwaka huu. Mwaka mpya unavyo anza, sisi hatupo wenyewe, sisi tuna Mama wa Mungu wakutusimamia na kutuongoza kwa kipindi cha mwaka mzima. 

Kati ya viumbe wote wa Mungu duniani na Mbinguni hakuna kitu wala mtu aliye karibu na Yesu kama Maria, Mama yake. Maria ni Eva mpya. Eva ni mama wa wanadamu wote ambaye alileta kifo kwa kukosa utii, lakini Eva mpya, Maria ameleta uzima au maisha kwa utii wake. Mt. Ireneo anamuita Maria kuwa sababu ya wokovu wetu. Cardinal Newman ambaye alilinganisha kati ya Maria na Eva “kama vile tulivyopata msahara wa dhambi kwa sababu ya dhambi, kwa njia ya Maria tunapata neema kwasababu ya Neema, kama vile Eva alivyokosa utii na Imani, Maria alitii na kuamini, kama vile Eva alivyokuwa sababu ya kusambaratika kwa vitu na kukosa uelewano, Maria ni sababu ya umoja na uelewano, Eva alisababisha Adamu aanguke, Maria alisababisha Mwokozi wetu azaliwe kati yetu, hivyo kwa zawadi ya Maria tumepata Baraka kubwa, hivyo kama Eva alivyosababisha dhambi kwa wote, Maria amesababisha neema kwa wote. Maria ni zawadi kubwa kutoka kwa Yesu kwetu sisi. Yesu alijua Mama yake ni zawadi kubwa kwetu sana.” Sikuu nzuri kabisa ya kumalizia oktava yetu ya Noeli, na kuanza mwaka huu mpya pia. 

Tutafakari leo, juu ya utakatifu ambao Maria alishirikishwa na Mwanae. Tunatafakari juu ya faraha kuu na Amani aliyokuwa nayo moyoni. Tutafakari juu ya hali ya juu aliyokuwa nayo isiyopimika. Mama wa Mungu atusimamie na kutuongoza kipindi cha Mwaka mzima na safari yetu yote ya maisha yetu hapa duniani. 

Sala: Bwana, ninaomba sala ya Mama Maria, zawadi ya upendo wa mama, iweze kuwa furaha yetu kipindi chote. Tunaomba mwitikio wake uliojikita katika unyenyekevu mkubwa, uweze kuwa ndani ya mioyo ya watu wako. Tunapo mheshimu Mama wa Mungu na Mama wa Kanisa, tunaomba muunganiko wetu na Mwanae utuletee wokovu. Yesu tunakutumaini wewe. Amina.

Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment