Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KUMTAFUTA YESU KWA MOYO WOTE!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Januari 11, 2024

------------------------------------------------

ALHAMISI, JUMA LA KWANZA

Somo la 1: 1 Sam 4:1-11 Wafilisti wanawashinda Waisraeli na kuchukuwa sanduku la Agano la Mungu.

Wimbo wa katikati: Zab 43:10-11,14-15,24-25 Tukomboe Ee Bwana kwasababu ya upendo wako.

Injili: Mk 1:40-45 Yesu anamponya mkoma.
------------------------------------------------

KUMTAFUTA YESU KWA MOYO WOTE!

Ushirikina ni kuviona vitu vina nguvu kuliko Mungu. Sanamu, medali, picha, masalia yana manufaa kama tutatumia kama nyenzo ya kutufanya tumkumbuke Mungu na watakatifu wake. Ni rahisi sana kusahau kazi yake na kutumia vitu vitakatifu vibaya. Ndivyo walivyo fanya Waisraeli katika somo la kwanza leo. Walitumia Sanduku la Agano kama ngao yao ya kuwakinga na kuwapatia ushindi katika vita. Walishindwa kutambua kwamba utiii kwa Mungu ni muhimu katika kuyatenda mapenzi ya Mungu. Ndivyo hivyo, sanamu, medali, picha, rozari, vinatukumbusha juu ya Kristo na Mama yetu Maria na kutuweka karibu zaidi na Mungu. Lakini ni wazi kwamba medali ya Mtakatifu Kristofa haina maana kama wewe unaendesha gari vibaya tu bila kujali. Huwezi kuvitumia vitumike badala ya upendo wako kwa Mungu na utii wa mapenzi yake, vitakuwa havina maana kwako kama lilivyokuwa sanduku la Agano kwa Waisraeli.

Watu wenye ukoma walitengwa kwa mujibu wa sheria ya Musa (Law 13: 44-46). Leo, tunaona mtu mwenye ukoma anamfuata Yesu. Sababu ya pekee ni kuwa, yeye kwa undani na kwa dhati anaamini kwamba Yesu anaweza kumponya. Alipiga magoti mbele ya Yesu na anasema 'Ukitaka, waweza kunitakasa.’ Alijua nini alihitaji, na pia ni nani wakumfuata. Alikuwa na imani kamili juu ya huruma na upendo wa Yesu.

Sisi pia, wakati mwingi tunasita sita kuenda karibu na Yesu. Kwanza, kwa sababu ya hali yetu ya dhambi; na pili sisi tunakuwa na wasiwasi kuhusu nini marafiki na familia zetu watasema. Sisi leo tunaitwa kumuiga mtu mwenye ukoma. Hasa kumkaribia Yesu kwa sakramenti ya kitubio tuipatanishe naye. Tunaitwa kumkimbilia Yesu, kwa kuwa yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa kutusamehe, kutuponya, kutupenda na kutufanya wazima kabisa.

Zaidi sana, miujiza kama hii, Yesu alipata umaarufu. Lakini hakuahangaika na umaarufu huo. Badala ya kubaki ili aendelee kupata umaarufu na kutambulika, alienda sehemu pa jangwa kusali lakini watu walimfuata huko pia. Alikuwa tayari kumwachia Mungu Baba wa mbinguni awalete kwake wale waliotaka wongofu wa kweli. Hili linapaswa kuwa kweli pia kwetu sisi. Ujumbe wa Injili wa kweli wakati mwingine pengine si ule ambao unaendana na tamaduni zetu maarufu zinazo tupendeza wenyewe. Yesu na Injili yake ya kweli haweki daima vichwa vya habari kama kwenye taarifa ya habari. Badala yake tunapaswa kumtafuta yeye, tunapaswa kumtafuta sehemu zilizo fichika na za ukimya ambapo anatusubiri. Ukimya huo upo wapi? “sehemu ya jangwa” anapo subiri? Je anakusubiri wapi ili mkutane naye? Mtafute ndani yako, ndani ya moyo wako na unapo mpata, utakuwa na furaha ya milele kwamba umejitahidi kumtafuta.

Sala: Bwana, ninakutafuta wewe, lakini nimetambua kuwa siwezi kutosheka nakusema inatosha katika kukutafuta wewe. Upo, ukinisubiri katika hali mbali mbali. Unaniita katika hali ya ukimya wa ndani na upekee. Katika sehemu za jangwa la maisha, unatamani kuilinda roho yangu. Nisaidie nikusikilize nakufanya safari ya kuja kwako. Na ninapo kupata, nifanye niwe na wongofu wa roho uliouweka katika akili yangu. Yesu nakuamini wewe. Amina


Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment