“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba 2, 2024
------------------------------------------------
JUMATATU, JUMA LA 1 LA MAJILIO
Somo la 1: Isa 2:1-5 Isaya anaongelea kuhusu maono kuhusu wakati wa mwisho wakati nyumba ya Bwana itakapo anzishwa, na watu wote watapata makao ndani yake.
Wimbo wa Katikati: Zab: 122:1-9 Jikabidhi kwa Mungu. Mpokee yeye katika maisha yako leo. Sali pamoja na Mzaburi.”Kama uso wako utatuangaza, sisi tutakuwa salama".
Injili: Mt 8:5-11 Yesu kwa kuamua kabisa anamponya mtumishi wa Jemedari. Kupenda kumponya kwake kunasababishwa na Imani kubwa ya Jemedari.
------------------------------------------------
SHAUKU YA KUMTAKA YESU
Kipindi cha majilio ni kipindi cha kuwa makini na kutumaini, tunatambua watu walio karibu na mbali watakao guswa na faraja yetu kwa utayari wetu kwao juu ya mahitaji yao, tunapo peleka mahitaji haya kwa Yesu, je, tunatarajia kwa ujasiri kabisa juu ya upendo wake na huruma yake? Kipindi hiki cha Majilio, tupo tayari, kumshangaza Yesu kwa uongofu wetu wa kweli na matendo mema, matendo ya huruma kwa ajili ya jirani zetu hasa wale waliotengwa na jamii?
Majilio ni kipindi cha wanadamu wote, lakini pia ni kipindi chetu wenyewe, ni kwa jili ya kila familia, kila parokia, kila jumuiya ya kitawa. Vidonda vya dhambi na maumivu ya hali ya mwanadamu vinalia pamoja na huyu Jemedari katika Injili leo: “Bwana, mtumishi wangu yupo nyumbani amepooza, akiugua kwa maumivu”.
Vipengele vingi vya hii Injili inayogusa vinashangaza. Tabia za kibinadamu, zinavuta ufahamu wetu vinashangaza na kutufundisha somo. Inashangaza kwamba hata jemedari mkubwa anaweza kumfikiria na kumhangaikia mtumwa.Wakati watumwa ni viwete, au ni mgonjwa wa kitandani au mikono haifanyi kazi, mtumwa ambaye hazalishi ilikuwa ni kumuuza sehemu nyingine ili akafanye kazi nyingine ndogo ndogo ambazo hazihitaji kuzunguka sana. Inashangaza kwamba huyu mtumwa aliyekuwa mgonjwa anapata huruma kutoka kwa bwana wake, aliye mheshimu, na kumpenda. Yesu alitambua fadhila ya huyu mtu. Huyu Jemedari huenda alikuwa ametoka katika upande wa jeshi la Syria aliye hamia. Hivyo alikuwa anatambua kwamba Yesu kama Myahudi ambaye ni mcha Mungu, pengine asingependa kuingia katika nyumba ya mtu wa mataifa, asije akajitia unajisi. Huyu jemedari anamwambia Yesu kwamba kikosi chake kinamtii bila shuruti imani yake ilimuongoza na kuamini kwamba Yesu alikuwa na uwezo wa “kuamuru” kutoka mbali ugonjwa wa mtumwa wake umuache. “Sema Neno tu na mtumishi wangu atapona”
Yesu akishangazwa na Imani ya Jemedari. Imani yake ni ya hali ya juu. Ni Imani iliomsukuma huyu Jemedari, ambaye sio Myahudi, kuamini kabisa kuwa atapona mtumishi wake. Jemedari huyu, akiamini kuhusu nguvu na mamlaka ya Kimungu alionayo Yesu juu ya mambo ya dunia, anatambua dhambi zake mwenyewe na kutostahili kwake Yesu aingie nyumbani kwake. Kwa kutambua madhaifu yetu pia, tunatubu kwa kurudia maneno ya huyu Jemedari kila wakati kabla ya komunyo wakati wa misa
Sala: Ee Mungu, tusaidie sisi tuweze kujiandaa kwa ujo wa Kristo Mwanao. Tunakuomba atukute sisi tukisubiri, tukiwa na shauku katika sala. Njoo Bwana kwetu, na ulete Amani. Tunatamani kufurahia katika uwepo wako na kukutumikia wewe kwa mioyo yetu yote. Yesu, nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2024 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment