“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba 23 , 2023
------------------------------------------------
JUMAMOSI, JUMA LA 3 LA MAJILIO
Somo la 1: Mal 3: 1-4, 23-24 Nabii Malaki anatabiri juu ya kuja kwa mjumbe ambaye ataanda njia ya Mungu kuja kwa watu wake.
Wimbo wa katikati Zab 24: 4-5, 8-10, 14 Mungu ni mwema na mweye haki. Anawaonesha njia waliopotea, anawaongoza wanyenyekevu katika njia iliyo sawa, anawafundisha maskini njia zake. Simama imara, niueni vichwa vyenu, kwasababu ukombozi wenu upo karibu.
Injili: Lk 1: 57-66 Luka anaelezea mazingira ya kushangaza ya kuzaliwa kwa Yohane Mbatizaji, mjuumbe ambaye alitabiriwa na nabii Malaki.
------------------------------------------------
KURUDI KWA BWANA!
Somo la Injili ya leo linaelezea kuhusu nafsi ya Zakaria, Baba wa Yohane Mbatizaji. Bwana alimbariki na Elizabeti kwa kupata mimba katika hali ya muuijiza kabisa katika uzee baada ya kuwa mgumba kwa siku nyingi. Malaika Gabrieli alifunua tukio hili la utukufu wakati Zakaria akiwa hekaluni, lakini Zakaria akakosa Imani. Na matokeo yake alipatwa na ububu mpaka siku ya leo ambayo Yohane Mbatizaji anazaliwa katika Injili. Injili ya leo inaelezea jinsi Zakaria anavyo funguliwa kifungo hichi cha kutokuamini. Anafanya hivyo kwa kufuata maelekezo ya Malaika kwa kumpa mtoto jina alilo ambiwa na Malaika kwamba atamwita “Yohane” na kwa namna ya pekee Zakaria na Elizabeti wanapewa nafasi ya kuonesha Imani yao kwa kukumbatia matukufu ya Mungu kwa kumpa mtoto jina walilopewa na Mungu. Katika hali ya kawaida tunaweza kusema kwamba “Zakaria” alibadilisha kosa lake”. Anabadilisha hali hiyo kwa kufanya jambo la Imani na kulifanyia kazi. Hili ni jambo la ushuhuda wetu kwetu wote kwasababu mara nyingi sisi wote tumekosa Imani sehemu Fulani katika maisha yetu.
Katika maisha yetu, tunaweza tukaonesha sehemu tulipo kosa Imani. Wakati mwingine anaona kutukumbusha kwa kutumia njia zake. Tunaweza tukapata matatizo Fulani wakati mwingine, lakini hii sio laana ya Mungu. Bali mara nyingi matokeo ya mateso yetu tunarudi na kujichunguza tena na kurudi kwenye Imani, na kutupa kitu kingine kikubwa zaidi alicho nacho Mungu juu yetu. Ndivyo ilivyokuwa kwa Zakaria alifungwa ulimi kwa wakati ili muda utakapofika aweze kukiri utukufu wa Mungu. Sisi tunapaswa tujilinganishe na yeye pia katika maisha yetu.
Injili ya leo pia inaweka alama ya jambo jipya. Kwa kuzaliwa kwa Yohane Mbatizaji, Luka anataka kutuonesha kwamba kipindi kipya kimeanza. Kipindi cha ahadi kimeisha, sasa hamna tena kusubiri, kipindi kimefika kwa ahadi hizo kutimia. Mungu ametimiza Neno lake. Mungu kwa upendo wake kwa wanadamu, anaingia katika maisha ya Mwanadamu. Kuingia kwa Mungu katika maisha ya Mwanadamu kunaleta furaha kwa wote.
Sala: Bwana, natambua kuwa ninakosa Imani katika maisha yangu. Nilishindwa kuamini yote uliosema juu yangu. Na mwishowe nikashindwa kuweka maneno yako katika matendo yangu. Bwana mpendwa, nikiteseka kwasababu ya madhaifu yangu, nisaidie nitambue kwamba mateso yangu yanaweza kuishia mimi kukupa utukufu na kubadili Imani yangu. Nisaidie kama Zakaria kufanya Imani yangu kuwa mpya daima, nikurudie wewe daima na unitumie mimi kama chombo cha Amani yako na cha kuleta kutukufu wako. Yesu, nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment