ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumanne, Novemba 21, 2023
Juma la 33 la Mwaka
Kumbukumbu ya kutolewa Bikira Maria Hekaluni
Zek 2:14-17;
Lk 1:46-55;
Mt 12:46-50
SADAKA ILIYO KAMILI!
Leo Kanisa linakumbuka siku ya kutolewa Bikira Maria Hekaluni katika Hekalu
la Yerusalemu. Inawezekana huenda manabii hawa watakatifu simeoni na Anna.
Walioshuhudia kutolewa kwa Yesu hekaluni, kama inavyo oneshwa katika sura ya
pili ya Injili ya Luka, huenda walimfahamu Mama wa Yesu akiwa msichana mdogo
hekaluni na kutambua ukweli wa utakatifu wake wa pekee. Kujiweka Bikira Maria
wakfu kwa Mungu kunaeleza sifa zote za sadaka ilio kamili: alikuwa tayari,
mkarimu, mwenye furaha, hakujuta, na hakujibakiza. Ni kwa jinsi ghani
ilimpendeza Mungu! Tunamuomba Mungu kujiweka kwetu wakfu kwake, kuweze kuwa
chini ya ulinzi wa Mama Maria tukisaidiwa na maombi yake yenye nguvu, na nafasi
yake ya pekee alio nayo kwa Mungu.
Katika somo la kwanza Mungu anatuambia tufurahi kwasababu anakuja kukaa
kati yetu. Katika Agano la Kale “binti Sayuni”, ilikuwa ni kati ya majina mengi
ya watu wa Mungu. Tunapo litumia leo katika Liturjia zetu tuna maanisha Kanisa,
lakini pia tuna maanisha Mama wa Mungu aliyekuwa karibu na Yesu na yeye ni
mfano kamili wa kutekeleza mapenzi ya Mungu. Katika Injili ya leo, tunasikia
Mama mmoja akimwambia Yesu “Heri tumbo lililokuzaa,” na Yesu anatumia muda huo
kuelezea thamani ya kuyafanya mapenzi ya Mungu. Nini maana ya “kufanya” mapenzi
yake? Kufanya mapenzi yake nikufanya kile unacho kifahamu kinaendana na mpango
wake. Neno lake linapaswa kuongoza katika mioyo yetu. La pili, yeye familia
yake ipo ulimwenguni mwote (familia ya Utatu katika Umoja). Wakristo wanapata
kuwa watoto katika familia hii, sio kwa kuzaliwa, bali kwakufanya mapenzi ya
Mungu. La tatu, kufanya mapenzi ya Mungu inatupasa kuwa na uhusiano mzuri naye.
Kitu kinacho haribu uhusiano wetu na Mungu ni dhambi. Ili kufufua uhusiano wetu
na Mungu lazima kukubali makosa yetu na kuachana nayo. Kwa maneno mengine,
tunapaswa kuungama dhambi zetu na kutubu. Mungu yupo tayari daima kutupokea ili
tufanye mapenzi yake , lakini tupo tayari kufanya mapenzi yake na kurudi katika
kundi lake?
Sala: Ee Maria, tufundishe jinsi ya kujitoa kama sadaka ilio hai kwa Mungu.
Amina.
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment