MASOMO YA MISA NOVEMBA
6, 2023
JUMATATU, JUMA LA 31 LA
MWAKA
_____________
SOMO 1
Rum. 11:29-36
Karama za Mungu hazina
majuto, wala mwito wake.
Kwa maana kama ninyi
zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepta rehema kwa kuasi kwao; kadhalika
na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema. Maana
Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.
Jinsi zilivyo kuu
utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au
ni nani aliyekuwa mshauri wake? Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye
atalipwa tena? Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena
vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
_____________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 69:29-30, 32-33,
35-36 (K) 14
(K) Kwa wingi wa fadhili
zako unijibu, Ee Bwana.
Nami niliye maskini na
mtu wa huzuni.
Mungu, wokovu wako
utaniinua.
Nitalisifu jina la Mungu
kwa wimbo,
Nami nitamtukuza kwa
shukrani. (K)
Walioonewa watakapoona
watafurahi;
Enyi mmtafutao Mungu,
mioyo yenu ihuishwe.
Kwa kuwa Bwana huwasikia
wahitaji,
Wala hawadharau wafunga
wake. (K)
Maana Mungu ataiokoa
Sayuni,
Na kuijenga miji ya
Yuda,
Na watu watakaa ndani
yake na kuimiliki.
Wazao wa watumishi wake
watairithi,
Nao walipendao jina lake
watakaa humo. (K)
_____________
SHANGILIO
Zab. 119:105
Aleluya, aleluya,
Neno lako ni taa ya
miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.
_____________
INJILI
Lk. 14:12 – 14
Yesu alimwambia yule
aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako,
wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije
wakakualika wewe ukapata malipo. Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema,
viwete, vipofu, nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana
utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Krist0.
_____________
Copyright © 2023,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment