MASOMO YA MISA NOVEMBA
3, 2023
IJUMAA JUMA LA 30 LA
MWAKA
_____________
SOMO 1
Rum. 9:1-5
Nasema kweli katika
Kristo, sisemi uongo, dhamiri yangu ikinishuhudia katika Roho Mtakatifu, ya
kwamba nina huzuni nyingi na maumivu yasiyokoma moyoni mwangu. Kwa maana
ningeweza kuomba mimi mwenyewe niharimishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya
ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili; ambao ni Waisraeli, wenye kule
kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu,
na ahadi zake; ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya
mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
_____________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 147:12-15, 19-20
(K) 12
(K) Msifu Bwana, Ee
Yerusalemu.
Msifu Bwana, Ee
Yerusalemu;
Msifu Mungu wako, Ee
Sayuni.
Maana ameyakaza mapingo
ya malango yako,
Amewabariki wanao ndani
yako. (K)
Ndiye afanyaye Amani
mipakani mwako,
Akushibishaye kwa unono
wa ngano.
Huipeleka amri yake juu
ya nchi,
Neno lake lapiga mbio
sana. (K)
Humhubiri Yakobo neno
lake,
Na Israeli amri zake na
hukumu zake.
Hakulitendea taifa
lolote mambo kama hayo,
Wala hukumu zake
hawakuzijua.
Aleluya. (K)
_____________
SHANGILIO
Zab. 119:34
Aleluya, aleluya,
Unifahamishe nami
nitaishika sheria yako, nitaitii kwa moyo wangu wote.
Aleluya.
_____________
INJILI
Lk. 14:1-6
Yesu alipoingia ndani ya
nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale
chakula, walikuwa wakimvizia. Na tazama, mbele yake palikuwa na mtu mwenye
ugonjwa wa safura. Yesu akajibu, akawaambia wana-sheria na Mafarisayo, Je! Ni
halali kuponywa siku ya sabato, ama sivyo? Wao wakanyamaza. Akamshika,
akamponya, akamruhusu aende zake. Akawaambia, Ni nani miongoni mwenu, ikiwa
ng’ombe wake au punda wake ametumbukia kisimani, asiyemwopoa mara hiyo siku ya
sabato? Nao hawakuweza kujibu maneno haya.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo.
_____________
Copyright © 2023,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment