MASOMO YA MISA NOVEMBA
14, 2023
JUMANNE, JUMA LA 32 LA
MWAKA
_____________
SOMO 1
Hek. 2:23-3:9
Mungu alimwumba
mwanadamu ilia pate kutokuharibika, kwa mfano wake mwenyewe, ila ulimwengu
uliingiwa na muti kwa husuda yake Shetani, nao walio wa upande wake hupata
kuionja.
Bali roho zao wenye haki
wamo mkononi mwa Mungu, wala maumivu hayatawagusa. Machoni pa watu walio
wajinga walionekana kwamba wamekufa, na kufariki kwao kulidhaniwa kuwa ni
hasara yao, na kusafiri kwao kutoka kwetu kuwa ni uharibifu wao; bali wao
wenyewe wamo katika Amani. Kwa sababu hata ikiwa (waonavyo watu) wanaadhibiwa,
hata hivyo taraja lao limejaa kutokufa, na wakiisha kustahimili kurudiwa kidogo
watapokea wingi wa mema.
Kwa kuwa Mungu
amewajaribu, na kuwaona kuwa wamemstahili, kama dhahabu katika tanuru
aliwajaribu, akawakubali mithili ya kafara. Wakati wa kujiliwa kwao watang’aa,
na kama vimulimuli katika mabua makavu watametameta.
Watahukumu mataifa na
kuwatawala kabila za watu; naye Bwana atawamiliki milele na milele. Wenye
kumtumaini watafahamu yaliyo kweli, na waaminifu watakaa naye katika upendo;
mradi neema na rehema zina wateule wake.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
_____________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 34:1-2, 15-18 (K) 1
(K) Nitamhimidi Bwana
kila wakati.
Nitamhimidi Bwana kila
wakati,
Sifa zake zi kinywani
mwangu daima.
Katika Bwana nafsi yangu
itajisifu,
Wanyenyekevu wasikie
wakafurahi. (K)
Macho ya Bwana
huwaelekea wenye haki,
Na masikio yake
hukielekea kilio chao,
Uso wa Bwana ni juu ya
watenda mambaya,
Aliondoe kumbukumbu lao
duniani. (K)
Walilia, naye Bwana
akasikia,
Akawaponya na taabu zao
zote.
Bwana yu karibu nao
waliovunjika moyo,
Na waliopondeka roho
huwaokoa. (K)
_____________
SHANGILIO
Zab. 25:4,5
Aleluya, aleluya,
Ee Bwana, unijulishe
njia zako, unifundishe mapito yako.
Aleluya.
_____________
INJILI
Lk. 17: 1-10
Yesu aliwaambia
wanafunzi wake: Ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au auchungaye ng’ombe,
atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula? Je!
Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe
kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa? Je! Atampa asante yule
mtumwa, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa? Vivyo hivyo nayi, mtakapokwisha
kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya
tu yaliyotupasa kufanya.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo.
_____________
Copyright © 2023,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment