“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatatu, Novemba 13, 2023
Juma la 32 la Mwaka
Hek 1:1-7;
Zab 138:1-10;
Lk 17:1-6
KUWA CHANYA KATIKA ULIMWENGU HASI
Katika maisha yetu ya kila siku, tunajua kwamba maisha sio kila wakati ni shangwe tu. Wakati mwingine kuna mawimbi na tufani. Lakini wale walio na hekima huweza kupata furaha kwenye nyakati hizi.
Yesu anawaambia wafuasi wake kwamba vipingamizi vitakuwepo tu katika maisha. Lakini analenga kabisa kipingamizi ambao kila mfuasi wa Kristo atapata, ambao ni kupingwa kwasababu ya Kristo na Injili yake. Yesu pia anawaonya wafuasi wake wasiwe sababu ya kuwa kikwazao kwa wafuasi wengine wa Kristo. Anawambia kwamba wawe watu wakuwa na hali njema ya kukuwa katika Imani, ambayo itawasaidia kungoa mizizi ya dhambi na hali ya hofu katika maisha.
Hili linaanza kwanza kwakuwa mfuasi wa Kristo aliye jisimika katika Imani na mafundisho yake. Pili kuwa na mtazamo chanya kwa yote yanayopinga Injili. Hili litamsadia mtu kukumbana na matatizo kwa neema na msaada wa Roho Mtakatifu. Mwisho, mfuasi hapaswi kuumizwa na kushindwa, au kwa kukataliwa, anapaswa kuwa mfano wa kupenda na kuwa mfano wa huruma kwa wote. Na hivyo “watangaa kama nyota kwasababu watakuwa wanajitoa sadaka kuokoa maisha ya ulimwengu (Flp 2:15-16).”
Yesu anaongea kwa mfano wa kungoa mti na kuutupa baharini. Tukikutana na kitu kisichowezekana katika maisha yetu, tunapaswa kuamini juu ya nguvu ya Mungu ya kufanya yasiyowezekana. Yesu anakuita leo ulete mabadiliko katika ulimwengu wa sasa.
Sala: Bwana, mimi ni dhaifu, niongezee Imani, ili niweze kuikimbia dhambi na kutembea na wewe kama mfuasi. Ninakuomba niweze kuleta mabadiliko katika ulimwengu wa sasa. Yesu, nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment