Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

KUKABIDHI MAISHA YETU KWA MUNGU!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI” 
Tafakri ya kila siku
Ijumaa, Novemba 17, 2023
Juma la 32 la Mwaka

Kumbukumbu ya Mt. Elizabeth wa Hungaria, Mtawa

Hek 13: 1-9;
Zab 19: 1-4 (K) 1; 
Lk 17: 26-37.


KUKABIDHI MAISHA YETU KWA MUNGU!

Kumtafuta Mungu, kwa ajili ya ukweli binafsi wa kumtambua ni hali ya zamani kama umri wa ubinadamu. Lakini bado kumtafuta kunaendelea…. Sisi ambao tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, lazima tuendelee kumtafuta, kumtafuta kwa kufunuliwa kwa Mwana wa Mungu, na kuja kwa Ufalme. Yesu hatoi jibu kuhusu ni “lini”. Lakini anatoa jibu ni jinsi ghani ya kujiandaa kwa hiyo siku. Njia pekee ya kujiandaa kwa ajili ya Ufalme wa Mungu ni kuwa tayari kukana nafsi na maisha yetu kwa ajili ya kumpenda Kristo (Lk 17:33). Tunafanya hivi kwa kuishi si kwa ajili yetu bali kuishi kwa ajili ya Kristo (2 Kor 5: 15). Kama hatufuati hili na kama mtu hamchagui Yesu, njia ukweli na uzima, atakuwa kama mfu. Kama unaishi ndani ya Yesu na Yesu ndani mwako, hapo upo tayari.

Yesu anatutolea fumbo, akituambia kwamba kujaribu kuokoa maisha yako ni kuyapoteza. Lakini kupoteza maisha yako itakuwa ni kuyapata. Usemi huu unaenda kwenye moyo wa kuamini na kujikabidhi. Kama tutajaribu kuongoza maisha yetu kwa nguvu zetu na kujaribu kuyaokoa kwa nguvu zetu, mambo hayataenda. Kwa kutuita sisi tupoteze maisha yetu, Yesu anataka tukabidhi maisha yetu kwake. Anapaswa awe ni yeye anaye ongoza maisha yetu kwenda kwenye mapenzi yake. Hii ndio njia pekee ya kuponya maisha yetu. Tunayakomboa kwa kuruhusu mapenzi ya Mungu yatawale na kuachia mapenzi yetu. Jambo hili sio rahisi ni ngumu kwa mara ya kwanza. Ni vigumu kufikia ukamili wa kujiaminisha kwa Mungu kabisa. Lakini tukifanya hivyo utashangazwa kwani mipango ya Mungu ni mikamilifu zaidi ya mipango yetu. Hekima yake ni juu zaidi ya chochote na majibu yake kwa matatizo yetu ni makubwa kuliko tunavyoweza kudhani. 

Tafakari, leo, ni kwa jinsi ghani ulivyo tayari kukabidhi maisha yako katika huruma ya Mungu? Kama unaishi ndani ya Kristo na yeye ndani yako, basi wewe upo tayari? . 

Sala: Bwana, ninakupa wewe maisha yangu, mahangaiko yangu kuhusu wakati ujao. Ninakuamini wewe kwa kila kitu. Ninajikabidhi kwako. Nisaidie mimi niweze kukuamini kila wakati na kuja kwako kwa mioyo yote. Yesu, nakuamini wewe. Amina

Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment