Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

YESU ANALIA JUU YA YERUSALEMU


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Alhamisi, Novemba 23, 2023
Juma la 33 la Mwaka

1 Mak 2: 15-29;
Zab 50: 1-2, 5-6, 14-15 (K) 23;
Lk 19: 41-44.

YESU ANALIA JUU YA YERUSALEMU 

Albert Schweitzer ni mwanamuziki mkubwa kutoka Ujerumani, alikuwa mtoto wa mchungaji, mpiga kinanda maarufu. Alikuwa na astashahada ya falsafa na elimu ya Mungu. Akiwa na miaka 30, alisoma ujumbe mmoja wa Mmisionari mmoja kutoka katika gazeti kuhusu hitaji kubwa la madktari Afrika. Akiwashangaza wengi kwa kwenda Gabon, Magharibi ya kati mwa Afrika. Alitumia fedha zake kujenga eneo kwa ajili ya wakoma. Dr. Albert Schweitzer aliandika : "siku moja katika kuchoka kwangu nilijirusha katika kiti katika chumba ambacho kilikuwa cha kuongea na watu, na huku akilalamika! Hivi nilikuwa na upungufu ghani kuja kuwa daktari katika maeneo ya mateso kama haya? Daktari mmoja msaidizi akamjibu, ni kweli Dr, hapa duniani kuna mateso lakini sio mbinguni”. Baadae Dr. Albert Schweitzer aliandika “sijui mwisho wako utakuwa nini, mimi nina hakika na kitu kimoja: kati yenu watakao kuwa wenye furaha kweli ni wale waliogundua kutoa faraja na kutumikia”. 

Katika somo la kwanza tunamuona Mfalme Atioko akiwaamuru Wayahudi wote watolee sadaka miungu ya Kigiriki. Matiasi hakukataa tu kufanya hivyo bali kufanya hivyo. “ aliwaua Wayahudi waliosogea na kutaka kufanya hivyo. Alisema “mimi na watoto wangu na kaka na ndugu zangu tutaishi kadiri ya Agano la Baba zetu” (1Mak 2: 20). Katika Injili ya leo Yesu anaulilia mji wa Yerusalemu. Kilio cha Yesu ni ishara ya unabii. Kama nabii Elisha alivyo lia juu ya Israeli, kwa kutabiri mateso (2Falm 8:7-15), Yesu anafanya hivyo pia kabla ya kifo chake. Mji wa Yerusalemu ulikuwa na bahati baada ya bahati ya ukombozi wao, Amani na ukuu, lakini watu waliacha tu nakujilalia tu kama vile nafaka juu ya mchanga. Alivyo ukaribia na kuuona vizuri mji, alitambua mara moja kwamba watu wengi watamkataa na watakataa ujio wake. Alikuja kuwaletea zawadi ya uzima wa milele. Mbaya ni kwamba wengi walimkataa Yesu kwasababu ya kumuona sio muhimu na wengine walipata hasira juu yake na kupanga kifo chake. Yesu alikuwa haulilii tu mji wa Yerusalemu. Analia kwasababu ya ukosefu wa Imani ambao watu wengi wanayo. Yesu alitambua hili na lilimumiza sana na kumhuzunisha moyoni. 

Tutafakari leo juu ya kishawishi cha kuona Yesu sio muhimu na juu ya ujumbe wake. Ngoa hali hii ya kuto kumuona Yesu ni muhimu ndani mwako na amua kupanga upya kumtumikia na kushika mapenzi yake matakatifu kwa moyo wote. Kama Dr Albert, ambaye kwa moyo wote aliamua kuacha mambo mengi huko Ulaya na kuamua kuja kuwatumikia watu huku Afrika au Matiasi ambaye aliona ni bora kufa kuliko kuacha kumtii Mungu. Je, upo tayari kumkaribisha Yesu ndani ya moyo wako au unamkataa kama Yerusalemu walivyo mkataa? 

Sala: Bwana, ninaomba ungoe kitu chochote kisicho endana na mapenzi yako ndani ya moyo wangu. Unapo lia kwasababu ya dhambi zangu, ninaomba machozi haya yanioshe mimi na kunitakasa ili niweze kufanya wongofu wa kweli ukiwa kama Bwana wangu na mfalme wangu. Yesu nakuamini wewe. Amina


Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment