Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

YESU ANAPONYA!


“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatatu, Oktoba 30, 2023
Juma la 30 la Mwaka

Rom 8: 12-17;
Zab 67: 2,4,6-7, 20-21 (K) 21;
Lk 13: 10-17.


YESU ANAPONYA!

Yesu alikuja huku ulimwenguni kwa ajili ya utume. Mojawapo ya utume huu ilikuwa ni kuwaponya wagonjwa. Kila muujiza ulikuwa nitendo la upendo alilofanya Yesu kwa mtu aliyeponywa. Leo utamuona mwanamke ambaye alikuwa akiteseka kwa miaka kumi na nane na Yesu anamuonesha huruma kwa kumponya. Ingawaje ilikuwa nitendo la upendo moja kwa moja kwake, kuna mengi ya kujifunza kwetu sisi. Huyu mwanamke ambaye aliongozwa na Imani yake ilimfanya aende katika sinagogi na kukutana na Yesu. Kwa kuona hili Yesu anachukua jukumu la kumponza.

Huyu mwanamke katika hali ya kweli hakuwa anatafuta uponyaji, lakini Yesu alipomuona moyo wake ulimsukuma na kwenda kumponya. Ni sawa na sisi pia tutambue Yesu anajua tunahitaji nini, hata kabla hatujamuomba. Kazi yetu daima nikubaki waaminifu daima kwake na tutambue kwamba katika uaminifu wetu atatupatia kile tunacho hitaji hata kabla hatujamuomba.

Huyu mwanamke alisimama imara alipo ponywa. Hii ni alama kuonyesha nini maana ya neema kwetu. Wakati Mungu anaingia katika maisha yetu tunaweza tena kusimama imara. Tunaweza kutembea tena tukiwa na nguvu mpya na utu mpya. Tunatambua sisi ni wanani na tunaishi kwa uhuru katika neema yake.

Tafakari leo, juu ya ujumbe wa Injili. Mungu anatambua kila kitu tunacho hitaji na atajibu mahitaji hayo kadiri ya wakati wake. Na wakati atakapo tupatia neema yake tutawea kusimama tena kama watoto wake. Tafakari, je kwenda kwetu kanisani kunakuwa kama kwa yule mwanamke aliyeponywa? Au kwenda kwetu ni kwa ajili ya matendo ya nje, kutazama makosa yaliotendwa na wenzetu wakati wa liturjia?

Sala: Bwana, ninajikabidhi kwako na ninaamini katika huruma yako. Ninatumaini kwamba utunisaidia mimi niweze kutembea katika njia yako kila siku ya maisha yangu kwa ujasiri wako. Yesu, nakuamini wewe. Amina


Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com

No comments:

Post a Comment