“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Alhamisi, Oktoba 5, 2023
Juma la 26 la Mwaka
Neh 8: 1-12;
Zab 18:8-11;
Lk 10: 1-12
UFUASI MAANA YAKE UTUME
Mpango wa Mungu ni kuokoa watu kwa kutumia watu kama wao wenyewe, na pia
kuwaongoza watu kwa kutumia watu, kama wao. Mungu alimtuma Mwanae mpendwa,
aliyezaliwa na mwanamke, Mwana wa mtu, ambaye yupo kama sisi isipokuwa dhambi.
Yesu alizaliwa maskini, akafanya kazi kama mwana wa seremala, na alienda kwa
Yohane mbatizaji kubatizwa kama vile ana dhambi. Lakini kwa kukiona kifo chake
aliwachagua watu wengine waendeleze utume wake kwa ajili ya wokovu wa watu
wengine. Petro alikuwa karibu na Yesu sana. “Simoni Mwana wa Yohane, je
wanipenda mimi kuliko hawa? Alafu kulikuwa na Yakobo na Yohane ambao
aliwachukua pamoja na Petro, kushuhudia kungara kwake sura na baadae mateso
yake katika bustani ya Gestemane. Na pia kulikuwa na mitume wengine. Na mwisho
kabisa leo tunasoma kuhusu wale sabini na wawili. Wanapewa melezo jinsi ya
kuenenda katika utume wao waweze kuwa na mtazamo wa utume wao na yapi
wasitende. Imani na tabia njema ndicho kiini cha utume wao. Kwanza wasali
wamuombe Bwana wa mavuno, kusali ni kuweka matumaini yao kwa Mungu na tabia
njema ni silaha ya kupigana na mbwa mwitu au dunia wanayo pita.
Papa Greogori Mkuu, alisema kwamba amri kuu ya mapendo ilipaswa kutawala na
kungara kwa wajumbe wote wa injili. Upendo wao kwa kila mmoja utakuwa ni ujumbe
wenye nguvu. Sisi tukiwa ni wajumbe wa Kanisa tumechaguliwa na kutumwa kuwa
watu wa kutangaza habari njema. Na hivyo, tukiwa ni wajumbe katika kanisa maana
yake kumhubiri Kristo, kumfanya awe hai, na kumfanya yeye aheshimike katika
sehemu zote ambapo Injili inatangazwa, kuaminiwa na kukiriwa.
Tusisahau wito wetu na kujitoa kwetu. Meli ipo salama inapokuwa pwani na
kutulia lakini haikutengenezwa ili ikae pwani tu. Tuondoke sehemu tulipo kaa na
kusonga mbele, tukimchukua Yesu pamoja nasi, hasa kwa wale ambao hawamfahamu
bado na kwa wale wanao mhitaji.
Sala: Bwana Yesu, tufanye sisi wajumbe wako wa kweli. Yesu, nakuamini wewe.
Amina
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment