“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Alhamisi, Oktoba 9, 2025
Juma la 27 la Mwaka
Mal 3: 13-18, 4: 1-2
Zab 1: 1-4, 6 (K) Zab 40: 4;
Lk 11: 5-13.
OMBA, TAFUTA, BISHA HODI!
“Amini nawaambia, ombeni nanyi mtapokea, tafuteni nanyi mtapata, bisheni
hodi nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa kila aombaye, atapewa na kila atafutaye
atapata na abishaye atafunguliwa mlango” (Lk11:9-10)
Mara nyingi Injili ya leo yaweza kutokueleweka. Wengi hufikiri kwamba
tunapaswa kusali sana tena mno ndipo Mungu atakapo jibu sala zetu. Wegine
waweza kufikiri kwamba Mungu hajibu sala zetu kama hatuja sali ya kutosha. Na
wengine waweza kufikiri kwamba chochote tuombacho tunapaswa kuendelea kuomba
daima mpka pale ambapo tutapewa.
Ni kweli kwamba tupaswa kusali daima na kwa kujitoa. Lakini cha muhimu
kabisa cha kuelewa ni hiki: ni napaswa ni Sali kwa ajili ya nini? Hili ni
muhimu kwasababu Mungu hatatupa kile tunacho omba, haijalishi ni mara ngapi
umesali na kwa nguvu kiasi gani, kama hakipo kwa ajili ya mapenzi yake na
utukufu wake. Kwa mfano, kama mtu ni mgonjwa na anakaribia kufa na ni sehemu ya
mpango wa Mungu, wa Mungu mwenyewe wa kuruhusu huyo mtu afe, sala zote za
ulimwengu haziwezi kubadili hili. Badala yake, sala kwa namna hii humwalika
Mungu katika hali hii ngumu na kumjalia kifo kitakatifu. Hivyo sala sio hali ya
kumbembeleza Mungu mpaka atupatie kile ambacho sisi tunataka, kama vile mtoto
anavyoweza kufanya kwa mzazi. Bali tunapaswa kusali kwa ajili ya kitu kimoja tu
na ni kimoja tu….. “mapenzi ya Mungu yatimizwe”. Sala hazisaliwi ili
kubadilisha akili ya Mungu, ni kwa ajili ya kutubadili sisi na kukumbatia yote
ambayo Mungu ametuita tuyanfanye.
Wengine wanasema “nimeomba kwa muda mrefu sana, lakini hakuna hata kimoja
nimepewa” lakini katika kweli huwa tunatafakari na kujiuliza kama nimeomba kitu
sahihi? Je nina tambua thamani ya vitu ninavyo omba? Je, vitu nilivyo viomba ni
vya muhimu? Kama nitapewa je, nitaweza kuvitumia vizuri?
Mtoto asiye na meno anaweza kumuomba Baba yake mua. Je, Baba yake atampa?
Hapana. Baba atasubiri mpaka akue awe na meno ndio ampe. Nyani hafahamu thamani
ya dhahabu ulioshika. Lakini aweza kunyosha mkono kuomba, je utampatia? Hapana,
haumpi. Kwasababu unafahamu thamani yake! Ni katika hali hiyo tunaweza tusijue
tunanyoosha mkono kuomba nini, lakini Mungu anajua. Hii haimaanishi tusiombe
chochote tunacho penda. Tunaweza kuomba lakini kama hatuvipati tunavyo omba,
tusikatishwe tamaa. Mungu anajibu katika hali ambayo itakunufaisha na njia
ambayo itakufanya ulicho omba kisikutenge naye.
Sala: Bwana nisadie mimi daima nikutafute wewe na niweze kuongeza maisha
yangu ya imani kwa njia ya sala. Ninaomba sala zangu zinisaidie kupokea mapenzi
yako matakatifu katika maisha yangu. Yesu nakutumainia wewe. Amina.
Copyright ©2013-2025 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment