MASOMO YA MISA OKTOBA
30, 2023
JUMATATU, JUMA LA 30 LA
MWAKA
_____________
SOMO 1
Rum. 8:12-17
Kama ni hivyo, tu
wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili; kwa maana kama mkiishi
kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili
kwa Roho, mtaishi.
Kwa kuwa wote
wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea tena
roho ya utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa
hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya
kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; wa Mungu,
warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate kutukuzwa
pamoja naye.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
_____________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 68:1,3,5-6,19-20
(K) 20
(K) Mungu kwetu sisi ni
Mungu wa kuokoa.
Mungu huondoka, adui
zake wakatawanyika,
Nao wamchukiao huukimbia
uso wake.
Bali wenye haki
hufurahi,
Na kuushangilia uso wa
Mungu,
Naam, hupiga kelele kwa
furaha. (K)
Baba wa yatima na
mwamuzi wa wajane,
Mungu katika ko lake
takatifu.
Mungu huwakalisha
wapweke nyumbani;
Huwatoa wafungwa wakae
hali ya kufanikiwa. (K)
Na ahimidiwe Bwana,
Siku kwa siku
hutuchukulia mzigo wetu;
Mungu ndiye wokovu wetu.
Mungu kwetu sisi ni
Mungu wa kuokoa;
Na njia za kutoka
mautini. (K)
_____________
SHANGILIO
Ebr. 4:12
Aleluya, aleluya!
Neno la Mungu li hai
tena li na nguvu, li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Aleluya.
_____________
INJILI
Lk. 13:10-17
Siku ya sabato Yesu
alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. Na tazama, palikuwa na mwanamke
aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana,
hawezi kujinyosha kabisa. Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama,
umefunguliwa katika udhaifu wako. Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka
mara hiyo, akamtukuza Mungu.
Basi mkuu wa sinagogi
alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu akawaambia
mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku
hizo, wala si katika siku ya sabato. Lakini Bwana akamjibu akasema, Enyi
wanafiki, kila mmoja wenu, Je! Hamfungi ng’ombe wake au punda wake siku ya
sabato katika zizi, aende naye kumnywesha? Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa
Ibrahimu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa
afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato? Aliposema haya wakatahayari wote walioshindana
naye; mkutano wote wakafurahi kwa sababu ya mambo matukufu yaliyotendwa na
yeye.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo.
_____________
Copyright © 2023,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment