MASOMO YA MISA, OKTOBA
18, 2025
JUMAMOSI, JUMA LA 28 LA
MWAKA
SIKUKUU YA MT. LUKA,
MWINJILI
SOMO 1
2Tim. 4:10 – 17
Dema aliniacha,
akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike; Kreske amekwenda
Galatia; Tito amekwenda Dalmatia. Luka peke yake yupo hapa pamoja nami. Umtwae
Marko, umlete pamoja nawe, maana anifaa kwa utumishi. Lakini Tikiko nalimpeleka
Efeso. Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, na vile
vitabu, hasa vile vya ngozi. Iskanda, mfua shaba, alionyesha ubaya mwingi
kwangu; Bwana atamlipa sawasawa na matendo yake. Nawe ujihadhari na huyo, kwa
sababu aliyapinga sana maneno yetu.
Katika jawabu langu la
kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba
wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia
nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa
yote.
Neno la Bwana…
Tumshukuru Mungu.
________
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 145:10 – 13, 17 –
18 (K) 12
(K) Wacha wako, Ee
Bwana, wajulisha matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako.
Ee Bwana, kazi zako zote
zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi,
Wataunena utukufu wa
ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza
wako. (K)
Ili kuwajulisha watu
matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya
ufalme wake.
Ufalme wako ni ufalme wa
zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya
vizazi vyaote. (K)
Bwana ni mwenye haki katika
njia zake zote,
Na mwenye fadhili juu ya
kazi zake zote.
Bwana yu karibu na wote
wamwitao,
Wote wamwitao kwa
uaminifu. (K)
________
SHANGILIO
Yn. 15:1 – 9
Aleluya, aleluya,
Ni mimi niliyewachagua
ninyi, nikawaweka mwende mkazae matunda, matunda yenu yapate kukaa.
Aleluya.
________
INJILI
Lk. 10:1 – 9
Bwana aliweka wengine,
sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali
alipokusudia kwenda mwenyewe. Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi
ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno
yake. Enendeni; angalieni, nawatuma kama wanakondoo kati ya mbwa mwitu.
Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani. Na nyumba
yoyote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; na akiwamo mwana
wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu. Basi,
kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi
amestahili kupewa ujira wake. Msihamehame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.
Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele
yenu; wapozeni wagonjwa waliomo, waambieni Ufalme wa Mungu umewakaribia.
Neno la Bwana… Sifa
kwako Ee Kristo.
________
Copyright © 2025,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.

No comments:
Post a Comment