“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumatatu, Oktoba 6, 2025
Juma la 27 la Mwaka wa Kanisa
Yon 1: 1-17; 2: 10
Yon 2: 1-3,7 (R) 6;
Lk 10: 25-37.
KUCHUNGUZA UPENDO WETU
Leo katika Injili mwalimu wa sheria anamuuliza Yesu swali ambalo, sisi
tungeweza kujiuliza katika maisha yetu ya kila siku. “Bwana, nifanye nini ni
urithi Ufalme wa milele?” (Lk 10: 25). Yesu, lakini, tena katika hekima anajibu
kwa yale yalioandikwa katika Maandiko: ‘kumpenda Bwana Mungu wako na jirani
yako kama nafsi yako’ (rej. Lk 10: 27). Kupenda maana yake ni kujitoa kwa
wengine kwa yote tulio nayo na yote jinsi tulivyo. Kujitoa kusikiliza wengine
kujitoa kuelewa wengine na kuwa na subira kwa ajili ya wengine. Huo ndio
upendo. Upendo huu unakuwa na asili ya Kimungu tunapo ueneza zaidi kwa wale
walio tuumiza katika maisha au kwa wengine tusio waona hata macho kwa macho.
Upendo unakuwa na Mguso wa Kimungu tunapo toka njee kwenda kuwasaidia hata watu
tusio wafahamu. ‘Kama mtu mmoja anateseka, watu wote wanateseka naye, kama
mmoja anaheshimiwa, watu wote wanashiriki katika furaha yake’ (1 Cor 12: 26).
Hii ndiyo fadhila ya Msamaria mwema.
Ni rahisi kuwa mtu wa kuhukumu na kuwa mkali kwa wengine. Ukisikiliza magazeti
au kusikiliza taarifa mbali mbali huwezi kusikia mara nyingi jambo la kumsaidia
mtu sana bali mara nyingi ni kuhukumu. Ubinadamu wetu unaonekana mara nyingi
kuwa wakali kwa ajili ya wengine. Na wakati ambapo hatuwi wakali tunashawishika
kuwa kama makuhani- mlawi katika simulizi hili. Tunashawishika kufunga macho
kwa wale ambao wanahitaji msaada wetu. Cha muhimu ni kuonesha huruma na
kuuonesha katika hali ya juu. Tutafakari leo, juu ya wito aliokuitia Mungu
kukuonesha huruma. Mtakatifu Mama Teresa aliwahi kusema “…kama unapenda mpaka
kunakuwa na uchungu, hakuwezi tena kuwa na uchungu bali upendo zaidi”. Huruma
ni aina ya upendo ambao mwanzo inaweza kuumiza kwanza lakini mwishoni inaacha
upendo mtupu.
Sala: Bwana, nifanye mimi chombo cha upendo wako na huruma yako. Nisaidie
mimi kuonesha huruma pale ambapo ni ngumu katika maisha. Nisaidie nyakati hizo
wakati unani badilisha mimi kuwa chombo cha zawadi ya neema yako. Yesu,
nakuamini wewe. Amina
Copyright ©2013-2025 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment